Sunday, December 6, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mwili wa mtu mmoja asiyefahamika wakutwa ukielea juu ya maji katika eneo la daraja la Salenda jijini Dar es salaam.https://youtu.be/04oFDLaUA3U

Wenyeviti wa mikoa wa CCM wapongeza hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli za kubana matumizi na kuwashughulikia watendaji wazembe. https://youtu.be/j7LZOgN-yXo

Wananchi na viongozi wa CCM wilayani Sumbawanga wampongeza Rais Magufuli kwa kasi ya utendaji kazi wake katika kutatua kero za wananchi.https://youtu.be/19DHpHZC3X8

Wananchi mkoani Manyara waiomba serikali kuwakumbuka na kutoa misaada kwa wananchi walio na uwezo wa chini ili waweze kupata huduma za afya kwa kiwango stahili. https://youtu.be/EgGPhwz1qK4

Madini aina ya Almasi yenye rangi ya pinki ambayo ni adimu na ghari duniani yagundulika nchini mkoani Shinyanga. https://youtu.be/aqlWsW_NlbE

Mwanasiasa na kada wa CCM Mohammed Raza auomba uongozi wa CCM kukabidhi uenyekiti wa CCM kwa Rais Magufuli ili aendelee kufanya kazi yake vizuri.https://youtu.be/1uacZoDBCY4

Baadhi ya viongozi wa dini ya kiislam wajitokeza kumuombea dua Rais Magufuli ili aweze kutekeleza majukumu na ahadi zake alizotoa kwa wananchi.https://youtu.be/NeUEoUV2k1w

Wazee wilayani Tandahimba mkoani Mtwara waiomba serikali kutekeleza kwa vitendo sera ya matibabu bure ili waweze kuimarisha afya zao. https://youtu.be/aaVUpcYmx-8

Uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga waweka utaratibu wa usafi katika soko la manispaa hiyo jambo lililopokelewa kwa furaha na wafanyabiashara wa soko hilo. https://youtu.be/17VKchKGmb0

Mgomo wa madereva na wamiliki kutoa huduma ya usafiri waendelea kwa siku ya 3 kutokana na madai mbalimbali ikiwemo mkuu wa wilaya ya Kigoma kumpiga dereva.https://youtu.be/Rh7ORKGI6UQ

Katibu mkuu wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Alphayo Kidata,afanya ziara ya kushitukiza katika mabaraza ya ardhi ya wilaya za Kinondoni na Ilala na kugundua mapungufu kadhaa. https://youtu.be/659TtfQ__ro

Shirika la umeme la Tanzania TANESCO, limetoa siku saba kwa wateja wanaolihujumu shirika hilo kujisalimisha mapema; https://youtu.be/2M89tylMFBc

Wananchama wa CCM mkoani Mwanza wamempongeza Rais John Magufuli kwa hatua anazozichukua kutatua kero zinazo wakabili watanzania;https://youtu.be/RHNa_YqoXwY

Katibu mkuu wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi  Aliphayo Kidata ameshangwazwa na hali aliyoikuta katika ofisi za baraza la ardhi la wilayani ya Kinondoni; https://youtu.be/VBjwiDolQd8

Shirika la UNESCO limetoa ripoti inayoeleza kuwa mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa wanafunzi wake kubeba mimba wakiwa shuleni; https://youtu.be/SO_PpNOD3mU

Serikali imewaagiza wakazi waliojenga katika safu ya milima ya Uluguru mkoani Morogoro kuondoka mara moja kabla ya disemba 8 mwaka huu;https://youtu.be/tr2jyDF6C4Y

Wafanyabiashara wa soko kuu la Babati mkoani Manyara wamegoma kulipa ushuru kutokana na halmashauri kushindwa kuwaondoa wafanyabiashara wanafanya biashara nje ya soko hilo; https://youtu.be/YkOeH3ovcug

Wakulima wa zao la Maharage mkoani Kagera wameshauriwa kulima zao hilo kibiashara ili wajipatie kipato; https://youtu.be/TXb2qteEXgQ

Klabu ya Simba yenye masikani yake mitaa ya kariako jijini Dar es Salaam yaanza kujipanga kuelekea mchezo wake dhidi ya klabu ya Azam;https://youtu.be/nRaCBSQ_f6U

Baadhi ya wananchama wa klabu ya Simba tawi la Vuvuzela wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuwapatia kadi mapema za uanachama; https://youtu.be/XNM62_uYI_Y

Baadhi ya maafisa wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda  mkoani Katavi wasimamishwa kazi kwa tuhumza za ubadhilifu wa fedha;https://youtu.be/Kp9Z2nAmv5Q

Shirika la utangazaji Tanzania TBC, limetunukiwa tuzo  kwa kufata taratibu za utarishaji wa fedha kimataifa; https://youtu.be/J_Xu2Qi7YiI

Shirika la umoja wa kimataifa UN limelazika kupunguza wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma kutokana na msongomano mkubwa uliopo;https://youtu.be/bjEUTgQy05M

Idara ya Uvuvi mkoani Kagera imekamata na kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani zaidi ya milioni mia sita na arobaini na moja; https://youtu.be/UwXZlpjTt3s

Zaidi ya shilingi milioni thelathini zilizotolewa na TASAF awamu ya tatu kwa lengo la kuzipatia ruzuku kaya masikini mkoani Tabora zimerejeshwa TASAF bila kutumika kutokana na uzembe wa watendaji; https://youtu.be/HoqqLw9OX5g

Wananchi vijijini wameambiwa kutokubali kutoa malipo zaidi pale wanapotaka kuunganishiwa umeme; https://youtu.be/cXqH7F34I48

No comments:

Post a Comment