Wednesday, December 30, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Askari wawili wa jeshi la polisi wafariki dunia huku wengine wawili wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakifanyia dori kupinduka.https://youtu.be/41LXwrwVCdQ

Serikali imesema itaanza program maalum ya kitaifa ya upandaji miti kuanzia januari mwakani kwa ajili ya kuendeleza mazingira na uhai.https://youtu.be/JDgVYy-q23E
Siku chache kabla ya mradi wa mabasi ya mwendokasi kuanza kufanya kazi baadhi ya madereva wasio makini waelezwa kuharibu miundombinu ya mradi huo. https://youtu.be/_Umh1_T4qp8

Watuhumiwa 8 walioshitakiwa kwa kuhusika na upotevu wa makontena zaidi ya 249 bila kulipiwa ushuru bandarini wapandishwa kizimbani hii leo.https://youtu.be/KRoA9sQrhdU

Gari pekee la kikosi cha zimamoto manispaa ya Lindi lapata ajali wakati likipeleka huduma ya maji kwenye makazi ya viongozi.https://youtu.be/ED3X3DG52gQ

Rais John Magufuli ametua makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wapya katika ikulu jijini Dar es salaam. https://youtu.be/WKv0B35C8KI

Mchumi wa siku nyingi na mwenyekiti wa mstaafu wa CUF Prof.Lipumba aeleza hofu yake huku akisema huenda Tanzania ikakosa misaada ya wahisani kutokana na mkwamo wa kisiasa Zanzibar. https://youtu.be/vFBMPE21af4

Serikali imesema itahakikisha upatikanaji wa uhakika wa dawa na vifaa tiba katika hospitali za umma ili kuondoa kero za mda mrefu kwa wananchi kununua dawa kwa gharama kubwa. https://youtu.be/K3wCIRxBbzk

Waziri mkuu Kassim Majaliwa awatahadharisha wakimbizi wa Burundi waliohifadhiwa nchini kuacha tabia ya kuingia na silaha nchini kinyemela.https://youtu.be/IjRslLTN_U0

Naibu waziri wa Afya Hamis Kingwala afanya ziara ya kushitukiza katika hospitali ya Kitete mkoani Tabora huku akikuta mapungufu kadhaa na kutoa maagizo. https://youtu.be/e7wKp4m1Sos

Mamlaka ya mapato mkoani Morogoro yagawa mafuta ya kupikia kwa taasisi mbalimbali baada ya kukamatwa yakiingizwa mkoni humo kinyume cha sheria kwa kukosa kodi. https://youtu.be/BsQpYlBheSc

Je unafahamu umuhimu wa Wosia katika kupunguza migogoro katika miradhi? Fuatilia hapa ujuzwe na kuelimika na mengi. https://youtu.be/4ud9bV5cfyE

Waziri mkuu Kassim Majaliwa atoa siku 2 kwa Katibu tawala mkoa wa Kigoma kukamilisha uchunguzi juu ya ubadhilifu wa fedha;https://youtu.be/GhO_pSTthfo

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imetoa adhabu kwa kampuni tano za simu za mkononi nchini kwa kushindwa kusimamia usalama wa wateja wao;https://youtu.be/FrUEDd_enag

Wakazi wa kijiji cha Endeshi wilayani Karatu wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa wataalamu wa huduma za afya katika kituo cha afya kilichopo kijijini hapo; https://youtu.be/yfHM24fgyj0
Serikali yashauriwa kubadili sheria ya manunuzi pamoja na kuweka kipaumbele kwa utoaji zabuni kwa viwanda vya ndani kwa lengo la kuendeleza viwanda vilivyopo nchini; https://youtu.be/uEcHs0iIzw0

Mwanauchumi nguli nchini Prof. Ibrahim Lipumba amempongeza Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuimarisha uhusiano wa Tanzania na nchi za nje;https://youtu.be/IunWL_rBp88

Klabu ya Simba imesema ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na mwekezaji Mohamed Dewji kuwekeza katika katika klabu hiyo;https://youtu.be/vgYf6ENtC7w

Klabu ya Yanga imekumbwa na bomoa bomoa inayondelea jijini Dar es Salaam kwa uwanja wake wa Kaunda kubomolewa; https://youtu.be/-8q32KS_9G8

Televisheni moja ya nchini marekani imeandaa mdahalo kwa wagombea wa shirikisho la mpira dunia FIFA kwa lengo la kupata kiongozi bora atakayesimamia shirikisho hilo; https://youtu.be/OahMGZa3w58

Watu wanne wamefariki dunia na wengine watatu kunusurika kifo mkoani Mwanza baada ya Mtumbwi waliokuwa wakisafiria kupinduka;https://youtu.be/oxKF-EAcq8g


Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya makatibu wakuu na manaibu wakuu katika baadhi ya wizara na kuteua wengine wapya;https://youtu.be/lM8blu714Bw
Baadhi ya wananchi mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuingilia kati tatizo la kupanda kwa gharama ya huduma za maji mkoani humo;https://youtu.be/djysToHXTPA

Wawakilishi wa watu wenye ulemavu wameviomba vyombo vya habari nchini kuajiri wafanyakazi wanaoweza kutafasiri habari pamoja na vipindi kwa kutumia lugha ya alam

Shirika la viwanda vidogo nchini SIDO limeingia makubaliano na serikali ya Canada kuwapatia wataalamu wa kufundisha uanzishwaji wa viwanda vidogo hapa nchini; https://youtu.be/fcQJiwc2OWE

Serikali inatarajia kuanza programu ya kitaifa ya upandaji miti kuanzia januari mwakani ili kuendeleza mazingira na misitu nchini;https://youtu.be/YvD8kW7gf_0

Shirikisho la soka hapa nchini TFF limeiomba serikali kuliruhusu kuendesha michuano ya soka katika shule za misingi na sekondari;https://youtu.be/4LwNUdyLNoI

Klabu ya Azam imerejea kileleni mwa ligi kuu soka Tanzania bara mara baada ya kuitandika Mtibwa Sugar ya mkoani morogoro kwa goli 1 kwa 0;https://youtu.be/Jumt_f8bXdA

Serikali imeaomba watanzania kumuombea dua mchezaji Mbwana Samatta kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani;https://youtu.be/-AFntsWf9XE

No comments:

Post a Comment