Tuesday, December 29, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mvua kubwa iliyonyesha wilayani Rungwe imesababisha maafa makubwa baada ya kubomoa nyumba 23 na zahanati na pia ikiharibu mazao.https://youtu.be/rhdRMRtRiDE
Serikali yapiga marufuku biashara za uuzwaji wa matunda yaliyowazi na vyakula katika maeneno ambayo hayakuanishwa na wataalam wa afya.https://youtu.be/ZjQ3Nh1TNOU
Juhudi za makusudi zaelezwa kuhitajika ili kutokomeza mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanayotishia kutokea kwa uhasama kati ya makundi hayo wilayani Kilwa. https://youtu.be/HiwnZLj-20k 

Wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA wapinga kusidio la mwajiri wao la kutaka kuwapunguza kazi jumla ya wafanyakazi 250.https://youtu.be/wubBOw6B0es

Rais Magufuli awaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua hivi karibuni huku mawaziri hao wakiahidi mambo makubwa kwa taifa;https://youtu.be/MAeRULxkNb0
Serikali imesema iko tayari kuzungumza na wataalam wa tiba asili nchini kwa lengo la mashauriano juu ya kutangaza huduma zao kwenye vyombo vya habari kwa kufuata taratibu. https://youtu.be/4MtWBUoaaFo
Waziri wa maliasili na utalii Prof.Maghembe asema serikali haina mpango wa kuteketeza maelfu ya meno ya tembo na nyara nyingine zilizohifadhiwa katika ghala la serikali. https://youtu.be/_DoUBH2K04Q

Siku kadhaa baada ya serikali kuendesha zoezi la bomoa bomoa baadhi ya waathirika wa zoezi hilo waelezwa kujenga vibanda ili kujistiri.https://youtu.be/Q8F1OAOZlhQ

Serikali mkoani Mwanza imesema itawachukulia hatua kali wazazi wa wanafunzi waliofaulu watakaoshindwa kuwapeleka shule.https://youtu.be/xkjwozis-7A

Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela, amuomba waziri wa nishati na madini prof. Sospeter Muhongo kuingilia kati mkwamo wa upatikanaji wa umeme katika wilaya ya Kyerwa. https://youtu.be/eYkciJN-uN8

Wachimbaji wa wawili wa madini wasadikiwa kufukiwa na kifusi mkoani Mbeya. https://youtu.be/aahcIgP3GXE

Shirikisho la vyama vya tiba asili nchini laibuka na kukanusha taarifa zilizotolewa na jukwaa la tiba asili la kugomea agizo la serikali.https://youtu.be/TvgS7q4hCMc


Rais John Magufuli amewaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua hivi karibuni  kukamilisha baraza lake la mawaziri; https://youtu.be/FMSy8ReiYFE
Inaripotiwa kuwa jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za kukutwa na makosa toafuti ikiwemo ujambazi;https://youtu.be/szIZeiZ-zl8

Polisi 6 wanaotuhumiwa kwa mauaji ya watuhumiwa wa ujangili nchini wapandshwa kizimbani hii leo katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/_7cEAWS-UhQ

Mahakama kuu kanda ya Mbeya imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na mgombea wa CHADEMA dhidi ya mbunge wa Kyela na waziri wa katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe;https://youtu.be/qrLZsWccXHo

Watanzania wameshauriwa kuwekeza nchini ili kuhimarisha sekta ya uchumi;https://youtu.be/9QokCf6J6do

Klabu ya soka ya Yanga imevunja mkataba na mchezaji wake wa kimataifa toka nchini Rwanda Haruna Niyonzima; https://youtu.be/mGnn7r7V2mY

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona, Xavier Hernández amesema kuwa mbinu za Jose Morinho zililenga ushindi pekee badala ya kujenda timu imara;https://youtu.be/q7cBMjRiKN

Wachimbaji wadogo wa dhahabu mkoani Mara wamemuomba waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo kuwapatia huduma ya umeme;https://youtu.be/FOSO-c3dte8

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaiagiza mamlaka ya bandari TPA  kukaa pamoja na wakazi Kibirizi na katosho mkoani Kigoma ili kutatua mgogoro uliopo baina ya mamlaka hiyo na wakazi  wa vijiji hivyo;https://youtu.be/33kjkqHAB_k

Inaelezwa kuwa ugonjwa wa kipindupindu unazidi kushika kasi jijini Mwanza huku idadi ya wagonjwa wapya wa kipindupindu wakiripotiwa kufikia 17;https://youtu.be/FMitS7rtz7I

Biashara ya mirungi mkoani Kilimanjaro imetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi mkoani humo;https://youtu.be/pVdUkbjVQNA

Serikali imewataka wamiliki wa viwanda vidogo vilivyopo jijini Dar es Salaam kuvisajili mara moja na kuanza kulipa kodi; https://youtu.be/Rm-EjWFyRWs

Baadhi ya wafanyabishara wa mchele jijini Dar es Salaam wamelalamikia kuwepo kwa idadi ndogo ya wateja katika kipindi hiki cha siku kuu;https://youtu.be/xyuMeuWjyQY

No comments:

Post a Comment