Thursday, December 3, 2015

KUPIGA PICHA NA KOMBE LA BARCLAYS PREMIER LEAGUE KESHO LITAKUWA IPP MEDIA, MLIMANI CITY, MAZESE NA BIAFRA

 Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Barclays hapa nchini, Osca Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ratiba ya kutembeza Kombe la Ligi kuu ya Uingereza limeanza kutembezwa jijini Dar es Salaam kuanzia leo  Disemba 3, mwaka huu
Na kesho wapenzi wa soka na ligi kuu ya Uingereza  waombwa kujitokeza kwaajili ya kupiga picha na kombe hilo ambalo limeaanza kutembezwa leo asubuhi. Ikiwa kwa kesho asubuhi Kombe hilo litaanzia katika tawi kuu la benki ya Barclays lililopo Posta na kuelekea katika ofisi za IPP Media  na baadae Mlimani City ambapo litakaa kwa muda wa lisaa limoja  na baadae Kinondoni Biafra, Mazese na kumalizia viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bidhaa wa benki ya Barclays, Valence Luteganya.
Meneja wa Bidhaa wa benki ya Barclays, Valence Luteganya kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kwa wananchi kuwa Kombe la Ligi kuu ya Uingereza kuanza kupiganalo picha kwa wapenzi wa soka jijini Dar es Salaam. Pia aliwasihi wananchi kufungua akaunti za mshahara katika benki ya Barclays ili waweze kujishindia tiketi mbili (2) za kwenda kuangalia soka la ligi kuu ya Uingereza bila gharama yoyote kwa kuwa gharama zote zitakuwa zimelipiwa na benki hiyo. Kuanzia kulia ni Mkuu wa mtandao wa matawi wa banki ya Barclays, Emmanuel Katuma, Mkurugenzi wa kitengo cha wateja binafsi Benki ya Barclays, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Barclays hapa nchini, Osca Mwakyusa.
Wafanyakazi wa Benki ya Barclays hapa nchini wakipiga picha ya pamoja na kombe la ligi kuu la Uingereza leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment