Tuesday, November 24, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mahakama kuu kanda ya Mwanza yatupilia mbali ombi la mawakili wa serikali la kupinga kusikilizwa kesi ya zuio la kuagwa kwa mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo. https://youtu.be/KR3iProCzRQ

Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu mkoani Kagera uongozi wa mkoa huo waanzisha operesheni maalum ya kupambana na ugonjwa huo.https://youtu.be/yoTtXpFrp2c

Kiwango cha maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi chaelezwa kupungua kufuatia utafiti uliofanywa na taasisi ya TACAIDS. https://youtu.be/RhXESfUUYag

Migogoro ya ardhi manispaa ya Mtwara Mikindani yaelezwa kuwa tishio kwa upatikanaji wa makazi ya huduma kwa wananchi jambo linalohitaji msukumo mkubwa toka kwa madiwani. https://youtu.be/oVgrxISVHzo

Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI asema kuanzia ijumaa wiki hii wataanza kukagua usafi katika jiji la Dare Es Salaam. https://youtu.be/cpnDkX86fkw

Kampuni ya Mantra inayofanya utafiti wa madini ya Uranium wilayani Namtumbo yatimiza miaka 5 bila ya kuwa na majeruhi kazini. https://youtu.be/ZQgur_WWdIA

Bohari ya dawa (MSD) yaelezea mchakato wake wa kuharakisha upatikanaji wa dawa katika maeneo mbalimbali nchini. https://youtu.be/MzhErUKgzqY

Wajasiriamali wadogo na wakati washauriwa kurasimisha biashara zao ili waweze kutambulika kisheria hali itakayo wawezesha kuendesha miradi na biashara zao bila usumbufu. https://youtu.be/mrQuT0NqhJ4

Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa TAMISEMI kujieleza kwanini mradi wa DART haujaanza kazi mpaka sasa; https://youtu.be/aXQVlOpMibw

Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel iliyoko jijini Dar es salaam wasitisha kwa muda kutoa huduma zao wakiutuhumu uongozi wa kampuni hiyo kwa unyanyasaji.https://youtu.be/vp9EoxFtZTk

Manispaa ya Kinondoni yaelezwa kukithiri kwa vitendo vya rushwa huku mkuu wa wilaya hiyo akitoa tahadhari kwa watendaji wake. https://youtu.be/fD-y6UIokoQ

Shule ya msingi Isemabuna iliyoko wilaya ya Bukombe mkoani Geita yafungwa kufuatia ukosefu wa huduma ya vyoo shuleni hapo. https://youtu.be/ACjcDii1H2s

Wakazi wanaozunguka kituo cha daladala cha Makumbusho walalamikia DAWASCO na Manispaa ya Kinondoni kwa kushindwa kuzibua mitaro jambo linalo waletea kero na hofu ya magonjwa. https://youtu.be/aUbTTC1IxHE

Raia wanne kutoka China wamefikishwa mahakamani mkoani Mbeya kwa makosa matatu ikiwemo kosa la kuhujumu uchumi wa Tanzania;https://youtu.be/_7e5188fw_8

Umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini MOAT washauriwa kutoa habari zenye ukweli na zenye  kuaminika ndani ya jamii; https://youtu.be/LDfmSgFPiLg

Katibu tawala mkoa wa Kigoma Mhandisi John Ndungru, amewataka walengwa wa mradi wa TASAF kuzitumia pesa hizo kwa malengo yaliyokusudiwa;https://youtu.be/QZmtF2uTzsA

Shirika la utangazaji Tanzania la TBC limepongezwa kwa kuwa shirika linalojali haki za watoto nchini; https://youtu.be/k8S73rmN8Eo

Wafugaji wa Vipepeo visiwani zanzibar wameiomba serikali iwashirikishe katika maonyesho ya utalii kwa lengo la kupata soko zuri nje ya nchi;https://youtu.be/jrjbgqjpx8w

Ofisi ya waziri mkuu imewashauri wakulima kutumia mifuko maalumu ya pics kuhifadhi nafaka kwa mda mrefu pasipo kutumia kemikali aina yeyote;https://youtu.be/XB-NNxaHTTE

Inaelezwa kuwa jumla ya kampuni 80 zinashiriki katika maonyesho ya bidhaa ya Syria yaliyoanza hii leo jiji Dar es Salaam; https://youtu.be/qqd_atMVX-A

Timu ya taifa ya Tanzania Kilimanjaro Stars imeendelea kugawa dozi katika michuano ya Challenge nchini Ethiopia kufuatia hii leo kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa 1 dhidi ya Rwada; https://youtu.be/11QGl303lxU

Afisa wa wanyama pori na mvuvi mmoja mkoani Singida wahukumiwa kwenda jela miaka 40 kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali; https://youtu.be/3HUfICSz86M

Mahakama kuu kanda ya Mwanza imehairisha kesi iliyofunguliwa na CHADEMA kuhusu madai ya kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo;https://youtu.be/tX6bL7tBdSc

Watoto wawili wa familia moja wamefariki na mwingine kujeruhiwa kufuatia nyumba waliyokuwa wamelala kuteketea kwa moto Mkoani Morogoro;https://youtu.be/wvmT_SPLXzE

Mkazi mmoja wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera akutwa  chumbani kwake akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba; https://youtu.be/gwk9KRomU9A

Shule ya msingi Bafanka Mkoani Geita iko hatarini kufungwa kutokana na vyoo kujaa hivyo kuhatarisha afya za wanafunzi; https://youtu.be/5lNmJ_h7uDM

Mbunge wa Singida Magharibi kwa tiketi ya CCM Mhe. Elibariki Kingu ameitupilia mbali posho ya vikao vya bunge na badala yake kutaka posho hiyo itumike kwa ajili ya maendeleo ya jamii katika jimbo lake; https://youtu.be/FPepOch755I

Vilabu vya ligi kuu na ligi daraja la kwanza nchini vimeelezwa umuhimu wa kufuata taratibu za leseni ili kuwa na sifa za kushiriki katika mashindano ya kimatafia;https://youtu.be/LNsbeCgNXCQ

No comments:

Post a Comment