Sunday, November 22, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMUTV: Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora yawahukumu Mh.Sakarambi na wenzake 2 kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kufanya mauaji.https://youtu.be/y1LdmixvM-c
SIMUTV: Katibu mtendaji wa tume ya utangazaji Zanzibar asema tabia ya wanahabari kutofuata sheria na katiba za nchi ni miongoni mwa sababu zinazochangia kukiuka maadili ya kazi zao hali inayosababisha migogoro na mifarakano katika jamii.https://youtu.be/6_jYgDQtMhU
SIMUTV: Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) yawataka wanafunzi wa elimu ya juu kulipa tozo ya kusimamia ubora wa elimu katika vyuo vikuu kama ilivyokuwa awali kwani ni kwa faida yao wenyewe. https://youtu.be/HDDNzGBcWiw  
SIMUTV: Watu elfu 70 wanaoishi katika vijiji 43 vya halmashauri ya Wilaya ya Iringa wanahitaji msaada wa haraka baada ya kukumbwa na baa la njaa.https://youtu.be/xp0d8flUGZY
SIMUTV: Wanachama wa kampuni za Bega Kwa Bega na BKB zilizopo jijini Mwanza zinazo jihusisha na uwezeshaji wananchi kiuchumi na ajira waipongeza hotuba ya Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa bunge. https://youtu.be/Ct5aQWXDXyQ
SIMUTV: Wananchi katika majimbo ya Lushoto Mkoani Tanga na Ulanga Magharibi Mkoani Morogoro wanatarajiwa kufanya uchaguzi wa wabunge hii leo kufuatia kuhairishwa hapo awali.
SIMUTV: Mahakama ya haki za binadamu ya Afrika imetupilia mbali ombi la kumuachia huru mtanzania Alex Thomas anayetumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya mahakama za chini kumtia hatiani kwa kosa la wizi wa kutumia silaha.https://youtu.be/-ujLaGosbSM
SIMUTV: Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoshiriki katika kuripoti habari za uchaguzi mwaka huu kuwa havikuwa na usawa, bali upendeleo na ubaguzi hali iliyo wagawa watanzania katika itikadi za vyama vya siasa. https://youtu.be/fCGvEMDdSbE
SIMUTV: Kadhi mkuu wa Tanzania awataka wazazi kushirikiana na walimu katika kufuatilia mwenendo wa maadili ya wanafunzi ili kuwajenga kielimu na kimaadili.https://youtu.be/dHalYFjAsAE

No comments:

Post a Comment