Monday, November 30, 2015

HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Wakazi mbalimbali mkoani Lindi wajumuika katika kufanya usafi wa mji huo huku msanii Mrisho Mpoto akiunga mkono juhudi hizo kwa kushiriki. https://youtu.be/mBCEkJQZauA  

Mkazi mmoja mkoani Lindi afariki dunia baada ya kuangukiwa na udongo wakati akichimba mchanga na kupelekea mkuu wa wilaya hiyo kusitisha shughuli za uchimbaji. https://youtu.be/LKuZvVb_arU   

Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT wawaomba wananchi na viongozi wote wa dinizote nchini kumuombea Raisi Magufuli ili aweze kuendelea na hatua anazochukua ili kuleta tija kwa wananchi.

Siku chache baada ya Azam tv kurusha habari ya wazazi na walezi nchini kushauriwa kutowabagua na kuwatelekeza watoto wenye ulemavu, baadhi ya wakazi wa Shinyanga wajitokeza kuwatembelea.

Walimu wa Shule za sekondari na msingi wilayani Sengerema mkoani Mwanza waandamana wakishinikiza serikali kulipa malimbikizo ya madai yao.  https://youtu.be/x0c-TsDUMac

Kampuni ya AZAM yafanya uchunguzi juu ya taarifa zinazosambazwa kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa makontena bandarini huku ikikanusha. https://youtu.be/vC-chXWKxAc

Chama cha walimu CWT mkoani Iringa kimeitaka serikali kulipa madeni ya walimu na kupandisha mishahara ili waweze kuendana na kasi ya Rais Magufuli. https://youtu.be/pvcCWhUihXs

Familia moja ya marehemu Ally Kondo Mkasi imelazimika kulala nje kwa muda wa wiki moja baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kubomolewa huku wakiutuhumu uongozi wa serikali ya mtaa kuhusika;https://youtu.be/55MdaU6Q9JE

Papa Franscis awasili Jamhuri ya Afrika ya kati huku akitegemewa kujaribu kusuluhisha mgogoro wa kidini ulioko nchini humo. https://youtu.be/EPOKobrpTnE

Umoja wa wananchi kutoka jumuiya ya nchi za Afrika mashariki ZINDUKA umetoa pendekozo la lugha ya Kiswahili itumike katika mijadala ya mikutano yote ya nchi za Afrika mashariki; https://youtu.be/10WgiXJ7zFA

Imeelezwa kuwa zaidi ya watu 1000 wenye vurusi vya UKIMWI katika halimashauri ya wilaya ya Iramba wamereja katika tiba baada ya kuacha kwa takribani miaka mitatu iliyopita; https://youtu.be/-tMnA09dZV0

Serikali imewaomba wazazi nchini kuwaruhusu watoto wao wa kike kushiriki katika michezo husuani mchezo wa mpira wa miguu; https://youtu.be/Q31s1wfjrSA

Wafanyabishara wengi nchini bado wanakabiliwa na ulewa mdogo kuhusu mikopo wanayokopa hali ambayo inawafanya washindwe kustawi ipasavyo. https://youtu.be/mmKY5mYPdUQ

Halimashauri ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora imesema italifanya kaburi la Mtemi Mirambo kuwa sehemu ya kivutio cha utalii; https://youtu.be/-R5OxdyHhnE

No comments:

Post a Comment