Monday, November 23, 2015

BENKI YA NIC YAIPIGA JEKI HOSPITALI YA MEDEWELL, ILIYOPO KIBAHA MKOANI PWANI

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Pankaj Kansara akiwa na mfanyakazi wa benki hiyo, Hamida Simbaulanga wakikabidhiana cheki ya shilingi 5,500,000 na  Afisa utawala wa hospitali ya Medewell, Amina Ramadhani, baada ya wafanyakazi wa benki ya NIC kutembelea Hospitali ya Medewell iliyopo Kibaha Mkoani Pwani.
  Afisa utawala wa hospitali ya Medewell, Amina Ramadhani akitoa maelekezo kwa viongozi wa benki ya NIC mara baada ya wafanyakazi wa benki ya NIC kutembelea katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki Kibaha Mkoani Pwani.
 Baadhi ya wagonjwa waliofika kupatiwa matibabu ya Mtoto wa jicho katika Hospitali ya Medewell iliyopo Kibaha Mkoani pwani. Na sehemu ya jicho iliyobandikwa kilebo ndilo jicho lenye tatizo la Mtoto wa jicho ndilo litakalo fanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo.
 Wagonjwa wenye tatizo la Mtato wa jicho wakiwa katika foleni ya kuingia kwa Daktali.

BENKI ya NIC imeipiga jeki hospitali ya Medewell  inayohudimia wagonjwa wa matatizo ya mtoto wa jicho bila gharama yoyote iliyopo kibaha Mkoani Pwani kiasi cha shilingi 5,500,000 ili kuweza kuhudumia wangonjwa kwa ufasaha zaidi na kupata matokeo mazuri kwa jamii inayopatwa na maradhi hayo. Ikiwa Ugonjwa wa Mtoto wa jicho huwapata zaidi wazee kwa kupoteza nguvu ya jicho kuona kwa ufasaha.

Benki hiyo imetoa msaada huo kwa wagonjwa 25 wanaosubiri kufanyiwa upasuaji pamoja na hospitali hiyo kuwa na wagonjwa 37 wenye matatizo hayo ikiwa kila mgonjwa anaghalimi dola za Kimarekani 100.


Akizungumza katika makabidhiano ya msaada huo Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Benki ya NIC, Pankaj Kansara  amesema kuwa benki hiyo imetoa msaada huo kwa kuwa wameona hospitali ya Medewell imejitolea kutoa huduma ya upasuaji wa wagonjwa wenye tatizo la mtoto wa jicho kutokana na hospitali hiyo kutoa huduma hiyo bila gharama yoyote.

Kwa upande wa wagonjwa wanaosubiri kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Medewell walishukuru madaktari wanaotoa huduma katika hospitali hiyo kuwa wanatoa huduma kwa upendo na kuwafariji pia ikiwa wakiwepo hospitali hapo wanapewa chakula na marazi bila kutoa huduma yoyote.

Ilibainika kuwa wagonjwa hao wanaosumbuliwa na tatizo la mtoto wa jicho ni kutoka sehemu tofauti tofauti hapa nchini, ikiwa ni Mwanza, Mheza, Tanga, Kilimanjaro na Kilwa.

Nae Afisa utawala wa hospitali ya Medewell, Amina Ramadhani  amewashukuru wafanyakazi wa benki ya NIC kwa kuona mahitaji ya jamii inayopatwa na matatizo ya Mtoto jicho.
Wafanyakazi wa Benki ya NIC wakipima kisukali katika hospitali ya Medewell iliyopo Kibaha Mkoani Pwani mara baada ya kutembelea hospitali hiyo. 
Viongozi wa benki ya NIC wakimsikiliza mkurugenzi wa Mradi wa hospitali ya Medewell, Shiraz Datoo. 
Wafanyakazi wa Benki ya NIC wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Medewell mara baada ya kukabidhiana cheki ya shilingi 5,500,000.
Viongozi wa beni ya NIC wakiagana na kiongozi wa Hospitali ya Medewell.

No comments:

Post a Comment