Monday, November 30, 2015

AZANIA BANK TAWI LA MOSHI YAKABIDHI VIFAA YA KUFANYIA USAFI KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI

 
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akikabidhi vifaa vya kufanya usafi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Jeshi Lupembe ,vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kutekeleza agizo la rais Magufuli la kufanyika wa usafi siku ya Desemba 9.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe akiwa ameongozana na Afisa afya mkuu wa manispaa hiyo,Mgeta Sebastian wakati wa kupokea msaada a vifaa vya kufanyia usafi kutoka Benki ya Azania tawi la Moshi.
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe akipokea rasmi msaada kutoka benki ya Azania uliowasilishwa na Meneja wa benki hiyo ,Hajira mmambe kwa ajili ya kufanyia usafi.
 
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe alipofika ofisini kwake kuitikia wito wa rais John Magufuli ya kufanya usafi Desemba 9 kwa kuchangia vifaa vya kufanyia usafi. 
 
Afisa afya mkuu wa manispaa ya Moshi,Mgeta Sebastian akisalimiana na Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe alipotembelea ofisi za halmashauri hiyo kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi. 
 
Meneja wa Azania Bank ,Hajira Mmambe akitia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.Jeshi Lupembe (kulia).
 
Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi,wakishusha mifagio ,iliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya shughuli za usafi zitakazofanyika Desemba tisa mwaka huu,kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi ,Jeshi Lupembe.


No comments:

Post a Comment