Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya Global Link Education imeendelea kupeleka
wanafunzi kwenda kusoma vyuo vya nje vilivyo na uwezo kutoa elimu bora.
Hayo ameyasema leo Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Global Link Education (GEL),Abdumaalik Mollel wakati
akitoa mafunzo kwa wanafunzi 65 wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya
juu.
Mollel amesema vyuo vya nje ambavyo
vinashirikiana na GEL vina ubora wa elimu pamoja na kuwa na vitendea kazi
vinavyoweza kufanya mwanafunzi afanye vizuri katika masomo yao.
Amesema wanafunzi 500, GEL imesha
wadahili katika vyuo vya nje na
wanafunzi hao wameona ubora wa vyuo hivyo na kuweza kuleta chachu ya
maendeleo nchini kutokana na utaalam wataopata huko.
Mollel amesema kuwa nafasi bado zipo
katika vyuo vya China hivyo wazazi wanaweza kuwasiliana na GEL kufanya usajili
katika vyuo hivyo.
“Nia ya GEL ni kuona wanafunzi
wanafanya vizuri katika matokea na tunafatilia tabia zao hatua kwa hatua tukiwa
na lengo ya kupata wasomi wenye ujuzi kwa maendeleo ya taifa”amesema Mollel.
Aidha amesema kuwa wanafunzi
wanaonyesha tabia mbaya wanawarudisha nchini katika kuweza kuokoa fedha za
mzazi kuendelea kuhudumia mtoto ambaye mwishoni hatafanya vizuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel akizungumza na wazazi na wanafunzi wanaotarajia kuondoka Oktoba 28 kwenda kusoma masomo ya elimu ya juu yalifanyika makao Makuu ya GEL leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi na wanafunzi wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya juu wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel hayupo pichani leo makao makuu GEL leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel ,akitoa nyaraka za taarifa za wanafunzi wanaokwenda nchini china leo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiuliza swali kwa masomo wanayokwenda kusoma katika vyuo vya nje leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel akizungumza na mzazi wa mwanafunzi wa anyekwenda kusoma nchini China,leo jijini Makao ya Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii
No comments:
Post a Comment