Thursday, October 8, 2015

MWENYEKITI wa chama cha DP mchungaji Christopher Mtikila azikwa kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa

MWENYEKITI wa chama cha DP mchungaji Christopher Mtikila amezikwa kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo.
Vilio vyatawala  huku aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi  watao ya Moyoni wasema alikuwa kiungo mhimu katika Taifa . 

Wakati Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji  Mutungi  akiwataka watanzania hasa viongozi wa vyama vya siasa kumuenzi Mchungaji Mtikila kwa kuenzi Amani wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu octoba 25 mwaka huu ,Filikunjombe asema mbali ya ukorofi wa Mtikila kwa kile alichokiamini ila kwake alikuwa ni mshauri mkubwa wa Ubunge wake katika jimbo la Ludewa.

Wakitoa salamu za rambi rambi wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika leo  kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa ,Jaji Mutungi alisema kuwa katika enzi za uhai wake marehemu Mtikila alikuwa akisimamia kile anachokiamini.

Alisema kuwa mbali ya misimamo yake ya kusimamia alichokiamini bado alikuwa ni mtu wa kujenga hoja na ambae hakupenda kuhatarisha Amani ya nchi hakuwa anapenda njia za mkato katika kupata majibu ya kile asichokiamini.

" Njia za mkato marehemu hakupenda kabisa kwani hata Kama jambo la kutisha ambalo wengine huogopa yeye alikuwa tayari kwenda mahakamani kusaka Haki yake bila kuhatarisha Amani ya nchi Mimi nafikiri kila mmoja akafuata misingi yake katika kudai Haki bila kuvuruga amani naamini tutafanikiwa.
" Alisema kuwa kuna mapungufu yanaweza kujitokeza ila Jambo la msingi kila mmoja kutanguliza kwanza amani ya nchi badala kuipa kisogo Amani na kupenda machafuko katika nchi".
Hivyo aliwataka watanzania bila kujali itikadi zao za vyama kuendelea na siasa huku wakitanguliza Amani ya nchi.
Mbunge aliyemaliza muda wake wa jimbo la Ludewa ambae ni mgombea Ubunge wa jimbo hilo Bw Filikunjombe alisema kuwa pamoja na Mchungaji Mtikila enzi za uhai wake alisimamia jambo ambalo 
alikuwa akiamini ila kwake amekuwa msaada mkubwa katika ushauri wa kuwatumikia wananchi wa Ludewa .
Alisema Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kumuunga mkono mbunge wa Ludewa ambae hakuwa msaada wa kimaendeleo kwa wananchi ila kwa upande wake alikuwa akimuunga mkono na hata kutosimamisha mgombea katika jimbo la Ludewa. 
" Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kuungana na mbunge asiyefanya Kazi za maendeleo jimboni Ludewa ila kwangu alikuwa akiniunga mkono na hata kunipingeza kwa Kazi nzuri ..... Kicho chake ni pigo kubwa kwa Taifa hasa kwa wana Ludewa ambao tulijivunia sana uwepo wake"

Hata hivyo alisema njia pekee kwake ya kumuenzi Mchungaji Mtikila ni kuendelea kuwatumikia vema wananchi wa Ludewa kwa kuleta maendeleo zaidi Kama alivyohitaji katika uhai wake.
Filikunjombe alisema katika kuamini kwake na kusimamia anachokiamini hadi mauti inamkuta alikuwa akitetea kuwepo kwa nchi ya Tanganyika na ndio maana kazikwa na bendera ya Tanganyika na kudai kuwa hakuna na kosa kupigania Tanganyika kwani Tanganyika inahitajika.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rerema Nchimbi alisema kuwa Mkoa wa Njombe umepoteza kiongozi makini na kuwa katika kumuenzi ni vema kwa vyama vya siasa kuendesha kampeni za amani na utulivu zaidi na kuwa wakati taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu ni vema kila chama kumuenzi Mtikila kwa kulinda Amani .
Naibu Katibu mkuu wa DP Taifa Abdul Mluya alisema kuwa suala la kifo cha mwenyekiti wake ni utata mtupu na bado wanaendelea kuchunguza.

Wakati huo huo Chopa ya Filikunjombe aliyotumia kufaria kwenda katika mazishi hayo iliwafanya wananchi kuacha kusikiliza Salam mbali mbali za viongozi na kukimbilia kutazama na kumlaki Mgombea huyo Ubunge jimbo la Ludewa.
 Mkuu  wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi kulia akiwa na Deo Filikunjombe mgombea  ubunge jimbo la Ludewa na mbunge aliyemaliza muda  wake katikati kushoto ni msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi leo  wakati wa mazishi ya Mchungaji Mtikila 
 Mchungaji Patrick Mgaya aliyekuwa  safari moja na marehemu Mtikila wa pili kulia akiwa katika mazishi hayo 
 Waombolezaji wakiwa msibani 

 Filikunjombe akitoa salamu zake wakati wa mazishi ya Mtikila 
 Wananchi wakimsikiliza Filikunjombe



 Filikunjombea akitoa mkono wa pole  kwa wafiwa  katikati ni mjane Mama Georgina  Mtikila 

 Filikunjombe akiwasili msibani kwa chopa 

 Jaji Francis Mutungi kushoto Bw MGaya na Askofu Mtetemela na Filikunjombe wakiwa msibani 
 Filikunjombe akijiandaa kubeba jeneza 

 Mjane  wa Mtikila  akiweka shada la maua 

No comments:

Post a Comment