Friday, October 9, 2015

MKUU WA MKOA WA MWANZA KUSHIRIKI ROCK CITY MARATHON

 Katibu wa idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani (wa pili kushoto), akipokea fomu ya usajili kutoka kwa Katibu wa chama cha riadha Mwanza, Peter Mujaya (wa pili kulia), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye jana alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za kilomita tano katika mbio za Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wanaoshuhudia ni Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Mwanza, Kizito Bahati (kushoto) na Mratibu wa mbio za Rock City Marathon kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bi. Adella Lamsa (kulia).
 Katibu wa idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani, akisaini fomu ya usajili kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye jana alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za kilomita tano katika mbio za Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wanaoshuhudia ni Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Mwanza, Kizito Bahati (kushoto) na Katibu wa chama cha riadha Mwanza, Peter Mujaya (kulia).
 Katibu wa idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani (kushoto), akionyesha fomu ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye jana alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za kilomita tano katika mbio za Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kulia ni mwakilishi wa New Mwanza Hotel ambao ni moja wa wadhamini wa mbio hizo, Senthil Kumar na Katibu wa chama cha riadha Mwanza, Peter Mujaya (wa pili kulia).
 Katibu wa idara ya utumishi Mwanza, Genzi Sahani, akisoma risala ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, jana jijini Mwanza muda mfupi kabla ya kuzindua usajili wa washiriki wa mashindano ya Rock City Marathon mbio za Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Mratibu wa mbio za Rock City Marathon kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bi. Adella Lamsa, akiongea wakati wa uzinduzi wa usajili wa washiriki wa mashindano hayo jijini Mwanza jana ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, alichukua fomu ya kujisajili kushiriki mbio za kilomita tano zitakazofanyika Novemba 15, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii mkoa wa Mwanza, Shaaban Luanda, akiongea wakati wa uzinduzi wa usajili wa washiriki wa mashindano hayo jijini Mwanza jana ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, alichukua fomu ya kujisajili kushiriki mbio za kilomita tano zitakazofanyika Novemba 15, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Na mwandishi wetu
Ikiwa ni siku chache kupita baada ya uzinduzi wa mbio za Rock City Marathon 2015, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo amekua mtu wa kwanza kujisajili kushiriki mbio hizo zilizopangwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizindua usajili wa ushiriki wa mbio hizo jijini Mwanza jana, Mulongo, aliyewakilishwa na Katibu idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Bw. Genzi Sahani, alitoa  wito kwa wanariadha nchini kujitokeza kwa wingi ili kuongeza ushindani wa mbio za mwaka huu, ambazo zimekuwa na lengo la kuhimiza utalii wa ndani nchini.

 “Nimekuwa mfuatiliaji wa mbio hizo tangu zilipoanzishwa mwaka 2009 na tumeshuhudia viwango vya mbio hizi vikipanda kila mwaka, kitu ambacho ni kielelezo cha kuonyesha maandalizi mazuri yanayofanywa kwa kuzingatia viwango na sheria zilizo wekwa,” alisema Mulongo katika shughuli hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa riadha.

Mulongo, alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni mchezo wa riadha umekua ukififia na kutaka wadau mbalimbali, ikiwemo makampuni binafsi, kuunganisha nguvu ili kuurudisha kwenye ramani mchezo huo ulioliletea taifa sifa kubwa katika miaka ya nyuma.

“Ni kweli kwamba makampuni na hata watu binafsi wanajitokeza kusaidia kukuza mchezo wa riadha hapa nchini, lakini bado mchezo huu una changamoto nyingi hususani katika mkoa wetu wa Mwanza na bado zinahitajika jitihada za ziada kwa wadau mbali mbali wa mchezo huu kushirikiana ikiwa ni pamoja na makampuni binafsi bila kusahau viongozi wa chama cha Riadha Mkoani Mwanza,” alisema.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Meneja wa Shirika la hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Mwanza Shaaban Luanda, ambao ni wadhamini wakuu, alisema: “Mbio za Rock City Marathon zimekuwa na mchango mkubwa katika kuinua mchezo wa riadha nchini. Sisi kama shirika la hifadhi ya jamii tunaamini kupitia michezo tunaweza kulinda afya ya jamii na ndio maana tumeendelea kudhamini mbio hizi.”  

No comments:

Post a Comment