Mahmoud Ahmad Arusha
WATANZANIA
500,000 wanatarajiwa kutembelea mbuga zote 16 za hifadhi za taifa mwaka
huu ikiwa ni hatua ya kuimarisha na kukuza utalii wa ndani ambapo
watajionea vivutio mbalimbali vilivyomo ndani ya hifadhi hizo.
Hayo
yameelezwa leo na Meneja uhusiano wa shirika la hifadhi za taifa,
Tanapa, (Pichani)Pascol Shelutete, makao makuu ya TANAPA, jijini ,Arusha,
alipokuwa akizindua hatua ya mwisho ya kampeni maalumu ya miezi sita
ya kuhamasisha Watanzania kutembelea hifadhi ili kujionea vivutio
kwenye hifadhi wanazopakana nazo ili kuimarisha utalii wa ndani
Kampeni
hiyo ni Makakati maalumu uliobuniwa na Tanapa, unaotoa hamasa kwa
watanzania kutembelea mbuga za hifadhi zilizopo karibu na maeneo yao kwa
gharama nafuu hasa siku za mwishoni mwa wiki na hivyo kuwapunguzia
matumizi ya fedha wanazotumia kwenye starehe na badala yake wazitumie
kutembelea hifadhi .
Meneja
uhusiano wa Tanapa, Shelutete, amesema kuwa kadiri miaka inavyozidi
kusonga mbele mwamko wa watanzania kutembelea mbuga za hifadhi
unaongezeka, ambapo mwaka 2013 watanzania 362,217, walitembelea hifadhi
zote 16 nchini, na mwaka 2014 watanzania 427,258 wametembelea mbuga hizo
.
Amesema
hatua ya mwisho ya uzinduzi wa kampeni hii inafanyika mkoani
Arusha,ambao unapakana na mbuga za hifadhi za Arusha, Ziwa Manyara na
Tarangire,na kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi 6 na itahitimishwa
Desemba mwaka huu.
Kauli
mbinu ya kampeni hiyo ni “Tembelea hifadhi uzwadike , akatoa wito kwa
watanzania kubadili mitizamo kwa siku za mwishoni mwa wiki zitumike kwa
ajili ya kutembelea hifadhi badala ya kuzitumia kwa ajili ya starehe
ambazo zinatumia fedha nyingi.
Uzinduzi
huo umeshirikisha wakuu wa Idara za utalii wa hifadhi za Tarangire,
Ziwa Manyara na hifadhi ya Arusha, pamoja na wadau ambao ni Chama cha
waongoza utalii nchini TATO,ambao kwa pamoja wameelezea manufaa ya
kutembelea hifadhi za taifa na sanjari kutatolewa zawadi mbalimbali kwa
watanzania watakaotembelea hifadhi hizo.
Tanapa mnatakiwa kufanya jitihada za kuwafanya watanzania wengi watembelee vivutio vya utalii na sio kukaa kutangza kuwa mnatarajia watu kiasi kadhaa kuhudhuria.Hivi sasa hapa arusha mmewewka vijana na mabango wakionyesha mbuga zetu hili si jambo baya ila mwatakiwa kuandaa safari rahisi kwa watanzania kuwawezesha kutembelea mbuga zetu na kuona vivutio.
ReplyDelete