Tuesday, September 1, 2015

WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAENDELEA KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA MAWASILIANO

  Ofisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo katika maduka ya Shoppers plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kushoto ni mteja wa kwanza kufika kupata huduma katika duka hilo Bw.Argylle Tsvakai na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.
 Mteja wa kwanza kufika katika duka jipya la Vodacom Tanzania Bw.Argylle Tsvakai (kulia) akiangalia moja ya simu zinazouzwa kwa bei nafuu katika duka hilo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa rasmi na Afisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (kushoto). Katikati ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (kushoto) akimmiminia mvinyo kwenye glasi Bw.Argylle Tsvakai ambaye alikuwa ni mteja wa kwanza kufika kupata huduma katika duka jipya la kampuni hiyo  lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa rasmi leo. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia. 
 Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimfanyia mahojiano Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia baada ya kuzinduliwa kwa duka jipya la kampuni hiyo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wadau wao walioshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo leo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

KATIKA  kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Mbezi Beach na maeneo jirani ya Tegeta, Kawe na Boko wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya  la kisasa katika  eneo la Mbezi Beach kwenye maduka ya Shoppers Plaza.

Mbezi Beach ni moja ya kitongoji maarufu katika jiji la Dar es Salaam ambacho kinakua kwa kasi kwa maendeleo na kuwa kivutio cha wawekezaji wengi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu na shughuli mbalimbali za kibiashara ikiwemo maofisi,mahoteli pia ni njia kuu ya kuelekea katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa M-pesa na uuzaji wa bidhaa  mbalimbali za Vodacom na litawawezesha wateja wa  Mbezi Beach na vitongoji vyake   wakiwemo wasafiri wanaoelekea na kutokea Bagamoyo  na wateja kutoka maeneo ya Kawe,Tegeta,  Goba na Mbezi juu.

Mtandao wa Vodacom unaongoza  kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika wilaya ya Kinondoni.

Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasliano wa Vodacom Tanzania, Rosalyn Mworia, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya  za kilimo klabu  na M-Pawa zinazolenga kuwawezesha kuwawezesha wananchi na kuwarahishia maisha.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Alisema Mworia.
Naye Mkazi wa Mbezi beach na Mteja wa kwanza kupata huduma katika duka hilo baada ya kuzinduliwa duka hilo aliipongeza hatua ya kusogezewa huduma karibu “Tunapongeza jitihada za kampuni hii inazozifanya katika kuwasogezea wateja wao huduma za mawasiliano karibu na makazi yetu kwani itatuwia rahisi kupata huduma kwa karibu badala ya kwenda mbali na huu ni uthibitisho kuwa hivi sasa jiji la Dar es Salaam linazidi kupanuka na huduma kuwafuata wananchi kwa karibu”.Alisema Bw.Argylle Tsvakai  mkazi wa Mbezi Beach.

Vodacom ina mtandao wa maduka 87 na wakala mbalimbali wa kuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la  88 kufunguliwa katika wilaya ya Kinondoni.

No comments:

Post a Comment