Thursday, September 24, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Mamlaka ya maji safi nchini kesho yaanza kusajili magari yanayotoa huduma ya maji safi pamoja na visima vya maji safi kwa lengo la kupunguza kuenea kwa kipindupindu.https://youtu.be/RkPXjA3f2NM

Wauzaji wadogo wa bidhaa za kampuni ya TBL waanza mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kibiashara ili waweze kua wajasiriamali ama wafanya biashara wakubwa.https://youtu.be/7ulki6Ncrck

Waumini wa dini kiislamu nchini waungana na waumini wenzao dunia kote kusherekea sikukuu ya eid el hajj wakifanya swala kwa pamoja. https://youtu.be/O77whWqiNC0

Katika hali ya kusikitisha mahujaji zaidi ya 500 wafariki dunia nchini Saudi Arabia kufuatia mkanyagano wakati wa ibada ya Hijahttps://youtu.be/YQljoACT3k0

Uongozi wa Ukawa wakataa kushiriki mdahalo wa wagombea uraisi huku ukisisitiza hauna mda kwa sasa. https://youtu.be/PAbxw_MYz48

Wafanyakazi wa migodini watakiwa kulinda uaminifu na uadilifu mahali pa kazi ili waweze kulinda ajira zao. https://youtu.be/F8m5L9EHUVE

Waandishi wa habari walia na ukata wa fedha za ripoti za uchaguzi jambo linalopelekea kukosekana kwa usawa katika utoaji ripoti za uchaguzi.https://youtu.be/iTa9DfOR5iU

Mahujaji takribani 717 waripotiwa kufariki dunia nchini Saudi Arabia baada ya kutokea mkanyagano wakati wa ibada ya Hija huko Makkahttps://youtu.be/djr9CBwLL44

Chama cha ACT wazalendo chalia na ukata wa fedha za kampeni za uchaguzi jambo linalokwamisha harakati za chama hicho. https://youtu.be/IvHMKbnDmfg

 Kila uchwao wananchi waelezwa kuwa na shauku kubwa ya kufuatilia kila kinachoendelea nchini zikiwa ni dakika za lala salama. https://youtu.be/JZE7qTOhR_s

Makamo wa raisi wa Tanzania Dr.Bialali asisitiza umuhimu wa amani huku akiwataka viongozi wa dini kuhubiri ili kuleta umoja wa kitaifa. https://youtu.be/qTxxXp1_Bn0

Timu ya Stand United chama la wana yatamba kufanya vyema katika michezo yake miwili ya hapa jijini Dar es salaam ikiwemo ya JKT Ruvu na Simba sports clubhttps://youtu.be/a1sept718UA

Timu ya Barcelona yakutana na aibu baada ya kupigwa kipigo cha goli 4-1 na timu ya Celta Vigo huku mshambuliaji Aspas akiingia nyavuni mara mbili. https://youtu.be/rs-V6RBk670

Mgombea mwenza wa uraisi wa CCM Bi.Samia Suluhu amaliza kampeni zake mkoani Tanga huku akinadi sera za CCM na kuhaidi kuboresha sekta ya afya.https://youtu.be/SEozDbLXPXs

No comments:

Post a Comment