Wednesday, September 30, 2015

NEC: HAKUNA WIZI NA UDANGANYIFU WA KURA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Kitaifa cha Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adili Mohamed wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Dar es Salamm Mohamed Chazi  wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akiteta jambo na Kamishna wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Vincent Msena wakati wa mkutano baina ya NEC na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu nchini uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Pwani Hussein Kibindu akisoma taarifa ya mada ya tathimini ya uchaguzi mkuu wa oktoba 25 mwaka huu wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Mwanza, Alfred Kapole akichangia mada wakati wa mkutano mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mkalimani wa lugha ya alama, Kudra Munishi akitoa ufafanuzi wa mada na hoja kwa watu wenye ulemavu wa kusikia wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA).

Na Ismail Ngayonga MAELEZO
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  imevitoa wasiwasi  vyama vya siasa  kuwa hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25 Oktoba, mwaka huu.
AIdha NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu aliokutana nao kwa ajili ya kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.

Jaji Lubuva alisema hadi kufikia sasa, vyama vyote vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo vimefanyika kampeni za kistaarabu ingawa katika siku za hivi karibuni baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa kauli na matamshi yaliyovuka mipaka, ambapo NEC imevionya vyama kuacha mara moja tabia hiyo.

“Vipo baadhi ya vyama vya siasa na wagombea wao  wamekuwa wakitumia muda mwingi kutoa lugha zisizofaa baada ya kunadi sera ya vyama vyao, vyama hivyo tumekutana nao na kuwataka kuacha mara moja kampeni za aina hiyo” alisema Jaji Lubuva.

Jaji Lubuva alisema tarehe 27 Julai mwaka huu, vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu vilisaini maktaba wa maadili ya uchaguzi huo, hivyo ni wajibu wa vyama hivyo kuzingatia viapo walivyotoa katika maktaba huo.

Akifafanua zaidi Jaji Lubuva alisema iwapo chama chochote hakina hoja ya kuzungumza na  wananchi ni vyema kikawa kimya hadi siku ya uchaguzi tarehe 25 Oktoba mwaka huu.
Aidha Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya kuingilia masuala ya utawala ya tume hiyo, kwani kwa kufanya hivyo vyama hivyo vitakuwa vikifanya kazi za tume hiyo na hivyo kuingilia masuala ya ndani ya kiutendaji ya taasisi hiyo.

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi huo, Jaji Lubuva alisema mahitaji yote ya msingi ya uchaguzi huo tayari yamepokelewa na NEC ikiwa karatasi, wino, na masanduku ya kura ambapo baadhi yake yameanza kusafirishwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kuhusu Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva alisema katika kipindi cha siku 10 zijazo kuanzia sasa Tume hiyo inatarajia kusambaza daftari la kudumu katika mikoa yote nchini na wananchi watatakiwa kuhakiki majina yao katika kipindi cha siku 8.

No comments:

Post a Comment