Thursday, September 3, 2015

EAGER WAKAA KUJADILI JINSI YA UNDELEZAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI

 Naibu Kiongozi wa Timu ya Shirika linanoshughulikia masuala ya Jotoardhi Afrika Mashariki (EAGER) Bw. John Heath akiwaelimisha wadau mbalimbali wa Kampuni inashughulikia Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) kuhusu Mifumo mbalimbali ya biashara kwa soko la Jotoardhi. Warsha inayofanyika tarehe 2-4 Septemba, 2015 jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi. Boniface Njombe akichangia mada katika warsha kuhusu Mifumo mbalimbali ya biashara kwa soko la Jotoardhi. Warsha iliyofanyika siku ya tarehe 2 Septemba, 2015 jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka Kampuni ya Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada kuhusu Mifumo mbalimbali ya biashara kwa soko la Jotoardhi, warsha iliyofanyika siku ya tarehe 2 Septemba, 2015 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka Kampuni ya Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Timu ya Shirika linanoshughulikia masuala ya Jotoardhi Afrika Mashariki (EAGER), Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya warsha iliyofanyika siku ya tarehe 2 Septemba, 2015 jijini Dar es Salaam.

PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWEGA-MAELEZO.

No comments:

Post a Comment