Wednesday, September 23, 2015

BADO MAHARI INA UMUHIMU MKUBWA KATIKA KABILA LA WAKURYA NCHINI TANZANIA

Kulia ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori Tarime Mkoani Mara akipokea Mahari ya binti wa Kaka yake kutoka kwa Mzee Samweli Chaha Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu, Tarime.

Na George GB Pazzo
Baadhi ya Watu wamekuwa wakiita ni zawadi inayotolewa kwa Wazazi ama Walezi pindi binti anapokuwa katika mipango ya kuolewa. Lakini kwa umaarufu wake, watu wengi wamekuwa wakiita Mahari.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na majadiliano makali juu ya dhana halisi ya Mahali. Hoja mbalimbali zimekuwa zikitolewa zikieleza kuwa suala la Mahari kwa sasa si la muhimu sana kama ilivyokuwa katika miaka ya zamani, hususani kwa baadhi ya makabila nchini ikiwemo kabila la Wakurya wanaopatikana Mkoani Mara ambapo wazee wa kabila hilo walikuwa wakipokea mamia ya ng’ombe kama mahari pindi mabinti zao walipokuwa katika mipango ya kuolewa.

"Kwa kabila la Wakurya bado suala la Mahari lina umuhimu mkubwa japo kumekuwepo na mabadiliko kidogo. Zamani binti wa kikurya alipokuwa akitaka kuolewa, Wazazi ama Walezi wake walikuwa wakipokea mamia ama makumi ya ng’ombe kama sehemu ya mahari",  Anaeleza mmoja wa wazee Wilayani Tarime na kuongeza;

"Lakini hivi sasa hali haiko hivyo tena kwani binti wa kikurya anaweza kuolewa kwa Mahari chini ya ng’ombe 10 ama pesa kati ya Shilingi Laki Nne hadi Milioni Moja na Laki Tano hii ikitegemea nafasi aliyo nayo binti. Mfano Mahali inaweza kupanda kama binti ni msomi, Mrembo ama mwenye nidhamu na maadili mema katika jamii".

Miongoni mwa maoni yanayotolewa na baadhi ya wanaharakati wa kutetea haki za binadamu yanakinzana na uhalali wa Mahari kwa misingi kwamba suala la Mahali limekuwa halichukuliwi kama zawadi na watu wengi na badala yake limekuwa likisababisha muoaji (Mme) kumnyanyasa muolewaji (Mke) kwa minajili ya kwamba yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho juu ya mkewe kwa kuwa tayari anakuwa amemlipia mahali ambapo hatua hiyo huondoa dhana kuwa Mahali ni zawadi na kugeuka kuwa kumtolea binti Mahali ni sawa na kumnunua ijapokuwa dhana hii inapingwa sana na watu wengi.

Hata hivyo baadhi ya Wazee kutoka Kabila la Wakurya Wilayani Tarime waliozungumza na Binagi Media Group wanaeleza kuwa bado suala la Mahali lina umuhimu mkubwa sana hususani katika Kabila la hilo la Wakurya na kwamba binti akitolewa mahali hueshimika katika jamii huku urafiki baina ya pande zote mbili za familia kwa maana ya Mme na Mke ukiimarika zaidi.

Je wewe una mtazamo gani juu ya Mahali kwani licha ya kuchukuliwa kama zawadi, baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa kumtolea binti Mahali ni sawa na kumnunua. Wasiliana nasi kupitia nambari +255 (0) 757 43 26 94 au barua pepe binagimediagroup@gmail.com


Tazama picha za Sherehe ya Mahali ya Milika Daniel Marwa Binagi Mzaliwa wa Kijiji cha Kenyamanyori kwa sasa akiishi Mtaa wa Rebu ambae anatarajia kufunga ndoa na John Samwel Chacha Kebasa mkazi wa Mtaa Rebu pia ikiwa ni Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

Wa pili Kulia waliokaa ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori Tarime Mkoani Mara akipokea Mahari ya fedha kwa ajili ya kumuoza binti wa Kaka yake aitwae Milika Daniel Marwa Binagi kutoka kwa Mzee Samweli Chacha Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu Tarime.
Mahari ikihesabiwa
Kushoto ni Professor Lloyd Binagi (Manamba) na Kulia ni Mzee Chaha Binagi wakihesabu pesa kwa jili ya Mahari ya binti yao
Baada ya Mahali kukamilika hatua iliyofuata ni familia ya mme na mke kusaini mkataba wa Makubaliano chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
Mkataba ukisainiwa
Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguti Rebu James Masoya akikabidhi Mkataba wa Mahari na Mzee Maina (Kushoto) ikiwa ni upande wa binti
Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguti Rebu James Masoya akikabidhi Mkataba wa Mahari na Mzee Samwel Chacha Kebasa (Kushoto) ikiwa ni upande wa mme
Sasa ni Msosi ambapo wageni upande wa binti wamekaribishwa na wenyeji wao upande wa mme
Sasa ni Msosi ambapo wageni upande wa binti wamekaribishwa na wenyeji wao upande wa mme
Wa kwanza kushoto waliosimama ndie Mkwe na hapo anatambulishwa Wazee
Picha ya Pamoja baina ya familia zote mbili kwa maana na mme na mke
Wazee wakibadilishana mawazo
Ndugu, jamaa na marafiki wakifurahia
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Wazee upande wa binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya kuchukua Mahari kufikia tamati
Ndugu upande wa Binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya Mahari kukamilika
Ndugu upande wa Binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya Mahari kukamilika
Hatimae wazee wakafika nyumbani na kufikisha habari njema kuwa Mahari imepokelewa na hapa wakaweka kumbukumbu ambapo Kutoka Kushoto ni Mzee Maina Binagi, Milika Daniel Binagi na mwanae, Mzee Chacha Binagi, Leah Daniel Binagi pamoja na Professor Lloyd Binagi

No comments:

Post a Comment