Tuesday, August 4, 2015

TASWIRA MBALI MBALI ZA MAONYESHO YA NANE NANE MKOANI LINDI

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (wa kwanza kushoto) akimsikiza Afisa Masoko na Uhusiano wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu (UTTPID) Kilave Atenaka (wa pili kulia) wakati mkuu huyo wa wilaya alipotembelea banda la taasisi hiyo leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. Kauli mbiu ya Manesho ya Nane Nane mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mwajuma Msina (kushoto) alipotembelea banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya Nane Nane leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. Kauli mbiu ya Manesho ya Nane Nane mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu (UTTPID) Mary Minja (kulia) leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Masasi (kushoto) akimsikiliza Mhasibu kutoka Idara ya Pensheni Wizara ya Fedha Imelda Mzatulla (katikati) wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi ambayo yanaongozwa na kauli mbiu “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”. Wa kwanza kulia ni Mchumi kutoka Idara ya Bajeti ya Serikali Wizara ya Fedha Prosper Fivawo.
Afisa Masoko kutoka taasisi ya UTT AMIS Waziri Ramadhani (wa kwanza kulia) akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na taasisi yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (kushoto) leo wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.

Afisa Habari kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila (kulia) akitoa maelezo kwa mmoja wa wageni waliotembelea banda la mamlaka hiyo. Afisa huyo alifafanua kuwa jukumu la kudhibiti masuala ya ki-usalama katika sekta ya usafiri wa anga nchini lipo chini ya mamlaka hiyo kwa sheria ya usafiri wa anga ya mwaka 2006 ambapo amewahamasisha Watanzania kutumia usafiri wa anga maana unatumia muda mfupi na ni wa haraka kufika eneo analokwenda abiria.
Afisa wa hali ya Hewa kutoka Pemba Suleiman Ali Juma akiwafafanulia wanafunzi kutoka shule ya Masingi Tulieni kata ya Mnazi Mmoja Mkoani Lindi namna mamlaka ya hewa inavyofanya kazi zake kwa manufaa ya Wanzania kujua masuala ya hali ya hewa kila siku. Wwakati mkuu huyo wa wilaya alipotembelea banda la taasisi hiyo leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. Kauli mbiu ya Manesho ya Nane Nane mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (wa kwanza kushoto) akishudia tairi ya akiba ya gari yake ikavalishwa cover mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF leo wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.

Kikundi cha sanaa cha Mundu Arts Group kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani wakionesha mchezo wa sarakasi kwa wananchi waliofika kujionea masuala mbalimbali leo wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Baadhi ya akina mama wakishiriki kazi za mikono katika shughuli za kukamilisha ujenzi wa mabanda yanayotumika wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Lindi)

No comments:

Post a Comment