Friday, August 7, 2015

Simu TV: Habari toka vituo vya televisheni

Mgombea uraisi kupitia ADC achukua fomu za kuwania uraisi katika ofisi za NEC huku akiitupia lawama UKAWA.

Polisi wilayani Busega wafanikiwa kudhibiti ghasia kati ya wafuasi wa Waziri  Dr. Titus Kamani na Dr.Chegeni kufuatia sintofaham matokeo kura za maoni.

Ujenzi holela na ule usio na mpangilio katikati ya jiji la mbeya waelezwa kuchagia jamii kushindwa kufikiwa na huduma za uokoaji kufuatia mbanano wa nyumba.

Tatizo la umeme mkoani Arusha laelezwa kuathiri sekta za uchumi na afya hivyo kuleta adha kwa wananchi

Shirikisho la wenye viwanda nchini labuni mbinu yakusaidia viwanda kupunguza matumizi ya gharama za nishati.

Wadau wengi wa soka watupa lawama kwa shirikisho la soka hapa nchini TFF kupendelea vilabu vikubwa kwa kusogeza mbele dirisha la usajili.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo azindua barabara ya Ndundu-Somanaga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 kwa kiwango cha lami.

Mwenyekiti wa UWT taifa Sofia Simba asema hana mpango wa kukimbia chama chake asema hayo akiwa mkoani Dodoma kabla ya kufungua kikao cha baraza kuu.

Mkuu wa mkoa wa Njombe DK. Rehema aishauri halmashauri ya mkoa wa Mbeya kujenga ushirikiano wa pamoja katika kulitumia soko la maharage la Uingereza.

Wananchi wakumbushwa kuwa makini na kujiepusha kuchagua watu wanaotumia fedha kama mtaji wa kupata uongozi.

Klabu ya Azam Fc yasema mabingwa wa soka wa Tanzania bara Yanga inahitaji kusajili wachezaji wawili wa klabu yao.

Mbunge waCCM wa Morogoro Mashariki Lucy Nkya,atuhumiwa kuwarubuni wanachama wa chama hicho kuhamia Ukawa baada ya kushindwa.
http://youtu.be/rzRIiOOq4ho                                                  

Kufuatia kujiuzuru kwa Prof.Lipumba nafasi ya uenyekiti wa CUF,viongozi wa chama hicho wilaya ya Ilemela wahamia ACT.
http://youtu.be/EgX17SfiXis                                                     

Hali tete yaibuka huko Mbarari kwa wafuasi wa CCM baada ya kuibuka na kudai kiongozi waliyemchagua siye aliyetangazwa mshindi.
http://youtu.be/YB6axKU0yqc                                                         

Raisi Kikwete asema licha ya juhudi za kukuza sekta ya kilimo nchini bado hakijaleta matokeo chanya ukilinganisha na nchi nyingine.


Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili Abdul Juma mkoani Geita apatwa na masahibu baada ya kutekwa na mtekaji kudai milioni 5. http://youtu.be/jSNYKuK_7VE

 Serikali yawataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara ili kuondoa mazingira ya magonjwa nyemelezi.http://youtu.be/8JJQqMcJlAk

 Serikali yaitaka halmashauri ya jiji la Mbeya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani maafisa ardhi kwa tuhuma za rushwa.http://youtu.be/WiF3S8ZW8xg

Licha ya jamii nyingi za vijijini kutambua samani ya kumiliki ardhi lakini wanakumbana na changamoto zinazokwamisha malengo yao. http://youtu.be/7_b0YEb_39E

 Moja vyuo vikuu vya nchini India cha furahishwa na hatua ya chuo cha usimamizi wa fedha IFM kuzindua kitabu cha utafiti.http://youtu.be/CuY-Xjv-Dkg

Chama cha mawakala wa forodha nchini Tanzania chaiomba serikali kukaa pamoja na chama hicho ili kusikiliza kilio chao juu ya utekelezwaji wa agizo la TRA. http://youtu.be/twvgLBNkuU8

 Serikali yaagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya malisho ya mifugo ili kuondoa migogoro ya mara kwa mara baina ya wakulima na wafugaji. http://youtu.be/zpjVm4JPm9I

 Timu ya soka ya Alliance School Of Sports Academy yategemewa kufanya vizuri katika michuano itakayo fanyika Rwanda ya shule za sekondari. http://youtu.be/4rlf7i7xAVI

 Kampuni ya vingamuzi ya Star Times yatangaza rasmi kuonesha live ligi kuu ya ujerumani maarufu kama Bundesliga.http://youtu.be/LqY3yEyl6yI

 Wasanii wa filamu nchini wametakiwa kukumbuka kuzingatia maadili wakati wote wanapotumia mitandao kupeleka kazi zao kwa jamii. http://youtu.be/z-oBD1QH27Q

No comments:

Post a Comment