Wasanii wa SHIWATA wakigaiwa maeneo ya kujenga katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga.
Wasanii wakipata maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib kabla ya kugaiwa nyumba zao katika awamu ya mwisho Agosti 8, mwaka huu,SHIWATA yazialika klabu, taasisi za michezo kujenga stadium, kumbi za burudani kijijini kwao Mkuranga,.
Bado kuna ekari 290 bado hajizapata matumizi
.Kila mwanachama kupewa robo hekari bure
.Jella Mtagwa, Dua Said, Hamisi Kinye ni baadhi yao.
Na Mwandishi Wetu
MIAKA 15 imepita sasa kutoka wasanii na wanamichezo walipoungana na kuacha itikadi zao kwa kuanzisha kikundi cha kufanya maonesho ya pamoja, kusaidiana kwa hali na mali na kutafuta makazi ya pamoja ya kudumu.
SHIWATA inayongozwa na Mwenyekiti Cassim Taalib katika kutimiza malengo hayo kutoka ianzishwe mwaka 2004 imekuwa ikiandaa matamasha mbalimbali katika ukumbi wa Star Light na Lamada mkoani Dar es Salaam na katika viwanja vya wazi kama vile Bandari Tandika na vingine kutika kuonesha sanaa ya wanachama wake.
Baada ya SHIWATA kusailiwa Baraza la sanaa Taifa(BASATA) mwaka 2005 pia imesajiliwa na Mamlaka ya Leseni (BRELLA) kwa shughuli za kiuchumi ikiwa na dira ya kuwakomboa wasanii kuwa na maisha bora kupitia mtandao huu ifikapo mwaka 2015.
Wasanii mbalimbali wa fani za maigizo, filamu, sarakasi, soka, bongo movie, muziki wa taarab,bongo fleva na kung Fu wamekuwa kivutio kikubwa kila yanapoandaliwa maonesho hayo.
Kipindi chote ambacho maonesho hayo yakifanyika SHIWATA ilikuwa ikihaha kutafuta njia nyingine ya kuwaendeleza wasanii wake kwa kutafuta eneo la kujenga nyumba za makazi ya wasanii ya bei nafuu na kupata shamba ambalo litalimwa kwa pamoja.
Mwenyekiti Taalib anasema katika jitihada za kutafuta maeneo zilianzisha msafara wa wasanii kutafuta eneo katika vijiji vya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Anasema katika jitihada hizo lilipatikana eneo la ekari 50 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe katika kijiji la Visegese ambalo uliingia dosari pale Serikali ya Wilaya ya Kisarawe iliyokuwa chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo wakati huo, Hanifa Karamagi kuwagomea wasanii kumiliki eneo hilo ambalo mpaka sasa fedha zilizolipwa zaidi sh. mil. 4.1 hazijarejeshwa.
Kipindi hicho baadhi ya wasanii waliokuwa mstari wa mbele ni pamoja na marehemu Steven Kanumba,Mwanzo Mpango "King Kikii", Suzan Lewis "Natasha", waandishi wa habari akina Maulid Kitenge, Peter Mwenda, Spear Patrick,Isaac Gamba na wengine wengi.
Taalib anasema baada ya kukwama kumilikishwa eneo hilo na Serikali ya Wilaya, jitihada za kutafuta eneo jingine ilianza na kufanikiwa kupata ekari 300 kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga mkoa huo huo wa Pwani.
Anasema Mkuu wa wilaya ya Mkuranga wakati huo, Henry Clemence aliwapokea kwa mikono miwili wasanii hao na kukubali kubariki kupatiwa eneo hilo kulikofanywa na uongozi wa Serikali ya kijiji cha Mwanzega.
"Jitihada ziliendelea a kutafuta mashamba ambayo wasanii watalima baada ya kuhamia kijijini na kufanikiwa kupata ekari 500 katika kijiji cha Ngarambe"anasema Taalib.
Anasema SHIWATA ilianza kusafisha shamba hilo kwa gharama kubwa na kugawa ekari tano kwa kila mwanachama iliyependa kulima lakini walishindwa kuliendeleza kutokana na sababu mbalimbali kama vile ulinzi wa mazao kutokana na wanyama waharibu.
Mwenyekiti Taalib anasema wanachama waliogaiwa shamba hilo ni wale wanachama hai waliolipia ada zao na kulipa sh. 200,000 kila ekari moja na kuongezewa nusu ekari kila mmoja.
Baada ya kugaiwa huko awamu ya pili ya kilimo kwanza katika shamba la Ngarambe ili kurahisisha baada ya kutumia mtambo wa kisasa (bulldozer) lililokodishwa kutoka Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kwa gharama y ash. mil. 22 kusafisha ekari 200.
"Ardhi hiyo ina rutuba kubwa na mazao yanayostawi eneo hilo ni mpunga, mahindi, mbaazi, viazi vitamu, ndizi, kunde, korosho, mtama na matunda kama embe, machungwa, matikiti maji na mafenesi"anasema Taalib.
SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 wa fani mbalimbali za sanaa za maigizo, mpira wa miguu, mpira wa wavu, netiboli, waigizai wa filamu, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, vijana na waandishi wa Habari wengi wao wameitikia ujenzio wa nyumba nafuu ambako mpaka Agosti mwaka huu nyumba 120 zimekwisha gaiwa.
Mbali ya maonesho ya sanaa, ujenzi wa nyumba za bei nafuu za sh. 631,000 zilizojengwa kwa miti kuezekwa kwa bati ni sh. 631,000, nyumba za chumba kimoja za saruji za sh. 750,000, nyumba za chumba kimoja na sebule sh. 3.8 na nyumba za vyumba viwili na sebule sh. mil. 6.4.
Serikali ya Wilaya ya Mkuranga ilikitambua rasmi kijiji hicho kwa kupeleka Mwenge wa uhuru Julai 21,2014 ukiongozwa kitaifa na Rachel Kassanda na wasanii zaidi ya 1,500 walijitokeza kupokea ugeni huo.
Mkuu wa wilaya hiyo kipindi hicho alikuwa Mercy Sila ambaye aalitoa ushirikiano katika sherehe za uzinduzi wa kijiji hicho kwa kuchonga barabara ya kufika kijijini na SHIWATA iligharimia kulipa minazi, miembe na miti ya matunda ambayo barabara ilipita.
Mwenyekiti pia anasema katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga wasanii wa fani ya filamu na tamthilia ilitengeneza filamu mbili ya kwanza ya kisufuria ambayo inaeleza maisha ya kawaida ya mtanzania na ya pili ya Ua Jeusi ambayo inaeleza ugonjwa hatari ambao bado haujajulikana ambazo zote zimeanza kurushwa kwenye vyombo vya habari.
Filamu ya Kisufuria imetengenezwa na wasanii maarufu kama Lumole Matovole "Big", Ahmed Olotu "Mzee Chilo", Haji Mboto na katika filamu ya pili ya Ua Jeusi ni Mzee Msisi na mwigizaji maarufu Kenyata.
Taalib anasema baada ya mafanikiop hayo changamoto iliwakuumba SHIWATA na wamiliki wa nyumba hizo kushindwa kuhamia kijijini jambo ambalo liliwalazimu kubuni njia nyingine ya kutoa ardhi nyiongine kwa ajili ya kulima bustani kwa wqale ambao watakuwa tayari kuhamia kijijini.
Katika mpango huo mwanamichezo maarufu, Dua said aliyewahi kuchezea Simba na timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", mchezaji wa zamani wa Yanga, Ramadhani Kampira na mwanamuzi mkongwe King Kikii kukubali kuhamia kijijini.
Hata hivyo wasanii 21 walijitokeza kuuungana na wanamichezo hao kuhamia kijijini Mwanzega, Mkuranga na kupewa chakula, mbolea ya kulima bustani ya mbogamboga na wameanzisha kilimo cha kisasa cha pamoja kijijini hapo.
Taalib anasema changamoto zinazoikabili SHIWATA mpaka sasa ni kutokuwa na vifaa vya kisasa vya kilimo kama vile matrekta kwa upande wa shambani, kutokuwa na barabara nzuri za kufika kijijini,kutokuwa na umeme, maji, kituo cha Polisi, shule na zahanati.
"Mpaka sasa ardhi ambayo imetumika kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi ni ekari kumi tu bado SHIWATA imebakiwa na hekari 290 ambazo zinahitaji uwekezaji wa klabu au taasisi kujenga viwanja vikubwa vya michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, mpira wa wavu, riadha na michezo mingine inayohitaji maeneo makubwa" anasema Taalib.
Anasema SHIWATA pia inawataka wanachama wake kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba zao, shule hospitali na wengine wenye wanaotaka kuchangia ujenzi watapata robo hekari yaani miguu 35 kwa 35.
Mwenyekiti Taalib anasema bado masharti ya kujiunga ni wale wale wanachama ambao ni wasanii, wanamichezo na wanahabari ambao wamejiunga na mtandao huo watapewa bure ardhi ya kujenga nyumba kutokana na uwezo wake.
Anasema mgao wa nyumba hufanyika mara mbili kwa mwaka, kila mwezi Desemba na mwezi Juni.Katika mgawo wa mwaka huu uliofanyika Agosti 8, mwaka huu ambapo nyumba 16 ziligaiwa na kufikisha nyumba 120 mpaka sasa.
Baadhi ya wacheaji wa zamani waliokabidhiwa nyumba zao ni mchezaji wa zamani wa timu ya Pan, Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania "taifa Stars, Jella Mtagwa, mcheaji wa zamani wa Simba, Dua Said na kipa wa Yanga, Hamisi Kinye.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisa Habari wa SHIWATA, Peter Mwenda 0715/0752 222677.
No comments:
Post a Comment