Thursday, July 2, 2015

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANG’ARA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA SABASABA

Mmoja wa wakina mama kutoka Kikundi cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania, (Tanzania Women Mining Association) Shamsha Diwani (katikati) akitoa maoni yake mara baada ya kutembelea banda la Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi Nchini ( TANSORT) kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi Nchini ( TANSORT) Dorcus Moshi (katikati) akiwaelimisha watoto waliotembelea banda hilo aina za madini yanayopatikana nchini Tanzania.
Baadhi ya wananchi wakiangalia aina za madini ya mawe katika banda la Wakala wa Jiolojia Nchini (GST), kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Banda la Wizara ya Nishati na Madini kama linavyoonekana pichani kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Uokoaji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Evarist Mwanakatwe (kulia) akielezea kazi ya uokoaji inavyofanywa na mgodi huo pindi yanapotokea maafa.
Mfano wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji katika banda la Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ulikuwa kivutio kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Afisa Uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Evarist Mwanakatwe (katikati) akielezea mikakati ya mgodi huo katika uimarishaji wa usalama katika shughuli za madini.
Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Philipo Mathayo (kushoto) akielezea sera ya madini katika kuimarisha shughuli za uchimbaji madini nchini.
Afisa Mawasiliano katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Suzan Mwita (kushoto) akitoa maelezo kwa maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini waliotembelea banda la mgodi huo.
Afisa Mazingira katika Mgodi wa Dhahabu (GGM) Paskazia Mwesiga (kushoto) akitoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira katika mgodi huo kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Steven Lowoko akiwaonesha wananchi jinsi umeme wa maji unavyozalishwa kupitia mfano wa mtambo wa kuzalisha maji kwenye banda la TANESCO.
Meneja Utawala Mfawidhi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) (Kulia) akielezea mafanikio ya mgodi huo kwenye banda la GGM.
Wataalam katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la TMAA.

No comments:

Post a Comment