Saturday, July 25, 2015

UZINDUZI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI AWAMU YA PILI WAFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA TEMEKE JIJINI DAR

 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid  (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya pili  katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema. 
 Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba (kulia), akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi huo.
 Mshauri wa masuala ya Afya ya Jamii kutoka Taasisi ya HBC, Mdadike Thabit (kulia), akimuelekeza jambo mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya watoa huduma kabla ya kufanyika uzinduzi huo.
 Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupata huduma za afya ya jamii kwenye uzinduzi huo.
 Wanamuzi wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia 
wakitoa burudani.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema akizungumzia mikakati ya Afya ya Jamii katika mkoa huo.



 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila, akitoa hutuba yake ya uzinduzi.
 Watoto nao walikuwepo kwenye uzinduzi huo.
 Mwanamuziki Juma Nature akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
 Wananchi walioshiriki uzinduzi huo.
Kiongozi wa kundi la muziki la Wanaume Family, Chege (kulia), akishambulia jukwaa katika uzinduzi huo.
Msanii wa kundi la utamaduni la HD Entertainment la Mbezi Beach, Michael Kamugisha, akiwa ameruka juu wakati wa kundi hilo lilipokuewa likitoa burudani katika uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

TANZANIA imeweza kufikia lengo la milenia namba 4 la kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili kutoka vifo 152 hadi 54 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid wakati akizindua kampeni ya awamu ya pili ya Wazazi Nipendeni katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana.

Alisema pamoja na kutofikia lengo la melenia namba 5 la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa robo tatu kufikia vifo 193 kwa kila vizazi hai laki moja, taarifa za umoja wa mataifa za mwaka 2014 zinaonyesha kuwa Tanzania imeweza kupunguza vifo hivyo toka 770 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 1990 hadi kufikia 410 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2014.

"Sababu zinazosababisha watoto waliochini ya miaka mitano kupoteza maisha ni kuharisha, nimonia na malaria na kuwa zinachangia takribani asilimia 50 ya vifo vya watoto hao waliochini ya miaka mitano" alisema Dk.Rusibamayila.

Alisema utapiamlo nao ni tatizo linalochangia vifo vya watoto hao kwani takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa kiwango cha udumavu ni asilimia 42 kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Dk.Rusibamayila aliongeza kuwa vifo vya watoto wachanga havijapungua kwa kasi inayoridhisha na vinachangiwa na wale watoto wanaozaliwa njiti, kushindwa kupumua vizuri mara baada ya kuzaliwa na maambukizi ya bakteria. 

No comments:

Post a Comment