Tuesday, June 23, 2015

SIMBACHAWENE ATAKA USHIRIKIANO ATEKELEZE MAJUKUMU YA WIZARA

  Waziri wa Nishati na Madini,  George Simbachawene, akizungumza na wananchi wa  Kijiji cha Mwilowe, Wilaya ya Mpwapwa, baada  kuzuia msafara wake   wakati  alipopita  katika Kijiji hicho wakati wa ziara ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili unaofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO). Wanakijiji hao walimweleza Waziri kuwa kijiji chao pia kiunganishwe na umeme.

 Wananchi wa Kijiji cha Mwilowe wakizuia msafara wa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakitaka kijiji hicho pia kiunganishwe na nishati hiyo. Waziri alikua katika ziara ya kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini unaofadhiliwa na wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).
 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akiangalia mfano wa mashine ya kusaga inayotumia umeme  wa mota aliyotengenezwa na Kijana katika Kijiji cha Lukole. Simbachawene aliahidi kumsaidia Kijana hiyo kuweza kufikia lengo lake.
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizindua Albam ya  nyimbo ya Kwaya ya Mtakatifu Agustino katika Kijiji cha  Kingiti, Kigango cha Kingiti, wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Pili.
 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akionesha Album ya nyimbo ya Kwaya ya Mtakatifu Agustino katika Kigango cha Kingiti, kijiji cha Kingiti baada ya kuzindua Albam hiyo. Simbachawene alizindua album hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Pili.
Waziri wa Nishati na Madini, George simbachawene akishiriki kucheza ngoma ya Kabila la Wagogo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Umeme Vijijini, Awamu ya Pili katika Kijiji cha Malolo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma.
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akimkabidhi baskeli , Diana Kalenza, katika kijiji cha Idodoma, Wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa  Umeme vijijini, Awamu ya Pili. Kwa mujibu wa Simbachawene baiskeli hiyo imetengenezwa na SIDO, Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi katika kijiji cha  Malolo akiimba wimbo  mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati wa ziara ya Waziri katika Kijiji chicho. Wimbo huo uliokuwa na ujumbe wa kumwomba waziri   kukiunganisha Kijiji hicho. Aidha, wimbo huo  ulieleza namna  wanakijiji hao  watakavyotumia nishati hiyo kwa maendeleo yao. 

Na Asteria Muhozya, Mpwapwa
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewataka wananchi kuwapa ushirikiano viongozi wa Wizara hiyo ili waweze kutekeleza kikamilifu majukumu yao kutokana na kusimamia rasilimali  muhimu  zinazobeba uchumi wa nchi.

Simbachawene aliyasema hayo kwa nyakati tofauti  wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini unafadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), na kutekelezwa na Shirika la Umeme   Nchini (TANESCO), katika vijiji vya Kinusi, Nzugilo, Idodoma, Malolo na Lukole, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma.

“Tuko kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Tunataka mshuhudie mafanikio makubwa ya usambazaji umeme vijijini. Serikali inatambua umuhimu wa nishati hii kwa maendeleo,na tutahakikisha kuwa, tunavifikia vijiji zaidi katika Awamu ya Tatu”, alieleza Simbachawene.

Simbachawene aliongeza kuwa, Mradi wa  usambazaji Umeme Vijijini ni endelevu na kuongeza kuwa, hivi sasa , serikali imezifikia takriban Kata na Tarafa  nyingi nchini na kuongeza kuwa, serikali itahakikisha inayafikia maeneo mengi zaidi yakiwemo yale yenye huduma muhimu za kijamii zikiwemo zahanati, shule na visima vya maji.

Aidha, alisema wizara yake iko kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote kuhakikisha kwamba wananufaika na rasilimali anazozisimamia bila kujali itikadi za vyama na hivyo kuwaomba wananchi kuonesha ushirikiano wakati serikali inapotekeleza Mradi huo wa usambazaji umeme Vijijini.

“Tuo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si kwa kuangalia  itikadi za vyama.Tutawatumikia wananchi wote bila kupokea rushwa kwa kuwa tunao uwezo wa kuwatumikia , nia tunayo, tunachotaka ni ushirikiano wenu”, alisema Simbachawene.

Katika hatua nyingine Simbachawene amepiga marufuku uchimbaji wa madini katika vyanzo vya maji na kueleza kuwa, wote watakaobainika kuchimba madini katika vyanzo hivyo, watafutiwa leseni zao za uchimbaji madini.

“ Sheria ya madini, kanuni na taratibu zake haziruhusu kuchimba madini katika vyanzo vya maji, kwa yeyote atakaebainika kuchimba madini katika vyanzo hivyo, tutamfutia leseni kwa kufuata taratibu na kanuni hizo”,alisistiza Simbachawene.

No comments:

Post a Comment