Friday, June 26, 2015

BENKI YA CRDB KUANZA KUUZA HISA STAHILI JUNI 26

 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifungua mkutano wa wanahisa wa benki hiyo katika Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akizungumza wakati wa mkutano wa wanahisa uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi yaWakurugenzi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na baadhi ya wanahisa wa benki hiyo kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa hisa stahili za benki hiyo unaoanza Juni 26 hadi Julai 16. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na baadhi ya wanahisa wa benki hiyo kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa hisa stahili za benki hiyo unaoanza Juni 26 hadi Julai 16. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na wanahisa wakimsikiliza Dk. Charles Kimei.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB. 
 Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na wanahisa wakiwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na mameneja wa matawi wakiwa katika mkutano huo.

Meza Kuu.

 Dar es Salaam, Tanzania
BENKI ya CRDB, imetangaza kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa Hista Stahili kwa wanahisa wake, unaofunguliwa Juni 26 na kuhitimishwa Julai 16, ili kuongeza mtaji wake wa uendeshaji.

Hisa Stahili ni zile za ongezeko zinazotolewa au kuuzwa kwa wanahisa wa benki hiyo kwa mfumo wa hisa moja mpya kwa kila hisa tano anazomiliki.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema kuwa baada ya maazimio ya wanahisa wake wote katika Mkutano Mkuu uliopita.

“Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, imeidhinisha kuingiza sokoni hisa mpya 435,306,432 kwa ajili ya wanahisa wake ambapo kila hisa moja itauzwa kwa shilingi 350, hivyo kusanyo tarajiwa la mtaji mpya litakuwa ni sh. 152,357,251,200,” alisema Dk. Kimei.

Alibainisha kuwa fedha hizo zitakazopatikana baada ya mauzo ya hisa zitatumika kwa mambo kadhaa, ikiwamo uboreshaji wa njia za kutolea huduma kwa wateja wa benki hiyo.

“Mwanahisa atakayekuwa na sifa za kupokea kupokea hisa hizi ni yule tu atakayekuwa kwenye kumbukumbu za vitabu vya benki mpaka kufikia Alhamisi Juni 18 mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya mwisho ukusanyaji kumbukumbu hizo,” alifafanua Dk. Kimei.

Aliongeza kuwa CRDB inahitaji kuongeza mtaji wake ili kufikia malengo yake ya kibiashara, ikiwamo upanuzi wa mtandao na ununuzi mitambo ya uendeshaji.


“CRDB imeona hii ndio njia sahihi na bora zaidi, kwani licha ya kuongeza mtaji, pia inatoa fursa kwa wanahisa wetu kuongeza hisa zao sambamba na umiliki wao wa benki hii,” alibainisha Dk. Kimei.

No comments:

Post a Comment