Friday, May 8, 2015

Mkutano wa 17 wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Mataifa ya Kusini mwa Bara la Afrika SADC wafunguliwa leo Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa 17 wa siku mbili wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Mataifa ya Kusini mwa Bara la Afrika SADC – SAC uliomalizika Zanzibar Beach Resort.
Kamanda wa Majeshi ya Anga wa Jamuhuri ya Botswana Meja General Mashinyana akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake waliotoka nje ya Tanzania kutokana na ukarimu walioupata Zanzibar wakati wa Mkutano wao wa Sadc – Sac.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Mataifa ya Kusini mwa Bara la Afrika SADC – SAC uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mzizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC – SAC mara baada ya kuufunga Mkutano wao Zanzibar Beach Resort.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Majeshi ya Anga pamoja na washiriki wa Mkutano wa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC – SAC mara baada ya kuufunga Mkutano huo Zanzibar Beach Resort.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Wakuu wa Majeshi ya Anga pamoja na washiriki wa Mkutano wa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC – SAC mara baada ya kuufunga Mkutano huo Zanzibar Beach Resort. Picha na OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Ushirikiano wa karibu unaozijumuisha Nchi za Jumuiya ya Mataifa ya Ukanda wa Kusini mwa Bara la Afrika SADC  katika masuala ya Ulinzi wa Anga umesaidia  kudhibiti  changamoto za Amani na Usalama ndani ya ukanda huo.

Alisema uanzishwaji wa Kituo cha pamoja cha uchunguzi wa usalama wa  Anga       { Exercise Blue Okavango } katika Mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo ya SADC  umeleta mafanikio makubwa.

Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akiufunga Mkutano wa 17 wa siku mbili wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika { SADC – SAC } uliokuwa ukifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mzizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

 Alisema ndoto iliyobuniwa na Viongozi wa Mtaifa wanachama katika kuanzisha    taasisi hiyo ya ulinzi wa pamoja wa Anga imelenga kuwajengea mazingira  bora ya ustawi wa kuishi kwa amani na utulivu  Wananchi wote wa ukanda wa Sadc.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kinachoongozwa na Kamanda Mkuu wa Kikosi hicho  Meja Jenerali Joseph Furaha Kapwani kwa kufanikisha vyema Mkutano huo wa 17 wa SADC – SAC hapa Zanzibar.

Akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki wa Mkutano huo wa 17 wa Sadc – Sac Mkuu wa Majeshi ya Anga wa Jamuhuri ya Botswana Meja Jenerali Mashinyana amewashukuru na kuwapongeza Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla kutokana na ukarimu waliouonyesha.

Kamanda Mashinyana alisema utulivu walioupata  yeye pamoja na Makamanda wenzake wa Mataifa wanachama wa Sadc – Sac wakati wakiwa Zanzibar umewapa faraja kubwa watayoendelea kuikumbuka katika maisha yao hata wakati wameshastaafu kazi ya ulinzi.

Washiriki wa Mkutano huo wa 17 wa siku mbili wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika { SADC – SAC } pia walipata fursa ya kutembelea sehemu mbali mbali za Kihistoria pamoja na maeneo ya matunda na Viungo.

No comments:

Post a Comment