Monday, April 27, 2015

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, LAZARO NYALANDU ATEMBELEA CHUO CHA USIMAMIZI WANYAMAPORI PASIANSI-MWANZA

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya kompyuta maalum zinazotumiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu akikagua moja ya vitanda na hema linazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akishuka kutoka basi linalotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akicheza na mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza wakinyanyua juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana,alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikwagua gwaride la heshima jana alipowasili Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu moja ya darubini zinazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya darubini zinazotumiw ana wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
Picha  ya pamoja ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza.

Serikali imesema kwamba itaanza kuwaajiri moja kwa moja askari wa wanyamapori kama inavyofanyika kwa jeshi la polisi na Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ).

Akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Wanyamapori cha Pasiansi jijini Mwanza jana Waziri a  Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema utaratibu unaotumika kw asasa unaleta usumbufu kwani urasimu unasababisha askari hao wanapomaliza mafunzo kusubiri kusailiwa wakati wa ajira wakati kuna upungufu mkubwa wa askari hao.

“Hatuwezi kukaa na kusubiri kupata kibali cha sekritarieti ya ajira kwa maana sasa hivi tumeanzisha Mamlaka ya Wanayamapori na kwa hiyo watakuwa na uwezo wa kuajiri mojakwa moja kuliko utaratibu wa sasa unaofanya mwanafunzi akimaliza chuo asubiri kusailiwa mbona polisi na jeshi hawafanyi hivyo?”

Waziri Nyalandu alisema kwa sasa kuna tatizookubwa kla ujangili na kuahidi kuwa vijana wengi watakaopata mafunzo wataajiriwa ili vita ya kupambana na majangili nchini ielekezwe sehemu zote ili kuweza kulinda na kuhifadhi rasilimali nchini kwa ajili ya vizazi vijavyo.

“Tumefanikiwa Serengeti na Selous lakini kwa sasa janga kubwa limekuwa katika pori la Rungwa ambalo limeungana na Ruaha, Tembo wengi wamekuwa wakiuawa na sasa vita tunaelekeza huko, ili kumaliza tatizo la ujangili”.

Alisema kuwa majangili watatafutwa popote wqlipo na kwamba wananchi wanatakiwa kuingia katika vita hiyo na kutoa taarifa zitakazosababisha majangili kukamatwa sehemu yoyote walipo ikiwa ni pamoja na ndugu zao na wafadhili wao.

Nyalandu ambaye alitembelea chuo hicho kukagua maendeleo ya mradi wa maboresho ya chuo unaofadhiliwa na Howard Buffet Foundation (HGBF) kwa kupitia taasisi yake ya uhifadhi ya Nature Conservation Trust aliagiza ujenzi wa bweni la wanafunzi 300 ukamilike katika kipindi kifupi kwa kuwa pesa za mradi zipo tayari.

Mkuu wa chuo hicho, Lowaeli Damalu alimshukuru Waziri Nyalandu kwa kutafuta mfadhili huyo na kusema kuwa kwa sasa chuo kimekuwa ch kisasa na vifaa vya kutosha kw akufundishia.

Alisema kwamba msaada huo unaokaribia Sh4bilioni umewezesha kununua vitabu magari, mahema darubini na kompyupa ambavyo unaweza kuwajenga wanafunzi kufanya kazi watakapoajiriwa kwa weredi mkubwa.

Dumalu alisema kwamba kwa sasa bwalo la chakula limekamilika na fedha kwa jaili ya ujenzi wa bweni ziko tayari lakini tatizo limekuwa ni kwa mkandarasi ambaye aliweka bei kubwa kupita bajeti na hivyo kumwahidi waziri kuwa mkandarasi ataletwa na mfadhili ili kukamilisha mradi huo kabla ya mwisho wa mwaka.

Alisema mbali na kuboresha mafunzo kwa wanafunzi lakini pia walimu wamepata fedha kutoka HGBF kwa ajili ya mafunzo kwa walimu na wafanyakazi ambao wamekuwa wakiendelea na mafunzo hayo kazini ili kuweza kupambana na ujangili na kwamba mradi huo bado unaendelea na kuwa mfadhili huyo tajiri namba mbili Marekani yuko tayari kuendelea kusaidia chuo hicho.

No comments:

Post a Comment