Wednesday, April 8, 2015

WAZIRI MAGUFULI AHUDHURIA MAHAFALI YA KUMI YA KIDATO CHA SITA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA CHATO

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mkoani Geita, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza wanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Chato wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao mwezi ujao.
Wanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Chato Mkoani Geita wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao mwezi ujao wakiimba wimbo maalum wa Shule hiyo katika Mahafali ya 10 shuleni hapo.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti mwanafunzi mmojawapo katika mahafali hayo.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kazi ya uchanaji wa mbao katika Shule ya Sekondari Chato. Mbao hizo hutumika katika kazi mbalimbali za ujenzi wa shule hiyo. Pia Dkt. Magufuli ameichangia shule hiyo kiasi cha Shilingi Milioni tano.
Waziri Magufuli akikagua moja ya computer katika shule hiyo.kushoto kwake ni Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mahendeka Mafele.
Dkt. Magufuli akipiga ngoma pamoja na kikundi cha Skauti cha Shule ya Sekondari Chato kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua vifaa katika maabara ya shule hiyo.
Waziri Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Chato Mwalimu Mahendeka Mafele kuhusu Ujenzi wa vyoo unaoendelea.
baadhi ya wazazi waliohudhuria katika mahafali hayo ya kumi ya kidato cha Sita shuleni hapo.
Vijana wanaotarajiwa kuhitimu kidato cha sita katika shule hiyo wakitoa burudani pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Bi Helena Busumilo.

No comments:

Post a Comment