mbunge Filikunjombe kulia na diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchilo wakifukia nguzo ya umeme
wananchi na mbunge wakisaidiana kufukia nguzo ya umeme
wananchi na mafundi wa umeme wakijiandaa kubeba nguzo |
mbunge Filikunjombe akishiriki kubeba nguzo ya umeme. |
wananchi na mbunge Filikunjombe wakiwa wamebeba nguzo ya umeme. |
katibu mwenezi wa CCM mkoa wa NJOMBE Honoratus Mgaya akichimba shimo la nguzo ya umeme |
mbunge Filikunjombe akitoka katika shimo baada ya kumaliza kuchimba shimo moja la mfano kama kuhamasisha wananchi kushiriki katika maendeleo
........................................................................................................................................
Na MatukioDaima BLOG Ludewa
WANANCHI
wa Ngalawale kata ya Ludewa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe
wameelezwa kufurahishwa na jitihada za kimaendeleo zinazofanywa na
mbunge wao Deo Filikunjombe na kukionya chama cha mapinduzi (CCM)
katika wilaya hiyo kutowaletea mgombea mwingine wa ubunge zaidi ya
Filikunjombe.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo ya Ludewa diwani wa kata hiyo
Monica Mchilo alisema kuwa toka jimbo hilo la Ludewa kuanza kuwa na
wabunge pamoja na kuwa kila mmoja ana jambo la kukumbukwa ambalo
amepata kulifanya katika jimbo hilo ila hakuna hata mbunge mmoja
kati ya wabunge zaidi ya watano waliopata kuongoza Ludewa ambae
amepata kutekeleza ahadi zake hata robo ya ahadi alizopata kutoa.
Diwani
Mchilo alitoa kauli hiyo leo wakati wa mkutano wa hadhara wa
mbunge Filikunjombe kuwapongeza wananchi hao kwa kukamilisha
uchimbaji wa mashimo ya nguzo za umeme katika kijiji chao .
Alisema
kuwa wakati mbunge huyo akiingia madarakani mwaka 2010 moja kati ya
ahadi yake ni kuhakikisha wananchi wa vijijini ambao wapo pembezoni
na mji wa Ludewa wanapatiwa umeme na kuwa kabla ya kumaliza muda
wake wa ubunge tayari ahadi hiyo imetekelezeka na ahadi nyingine
nyingi alizopata kuzitoa kwa wananchi wa jimbo hilo.
Hivyo
alisema kuwa inapendeza kuwa wana Ludewa kuendelea kumpa muda zaidi
mbunge Filikunjombe ili azidi kuleta maendeleo zaidi katika jimbo
hilo badala ya kuendelea kubadili wabunge kila wakati jambo
linalokwamisha maendeleo ya jimbo hilo na kuishia kuwapata wabunge
wasio na mapenzi mema na maendeleo ya wananchi.
'Ludewa
kwa miaka mingi tumeteseka kwa kumkosa mbunge mwenye uchungu
wa maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo ila kwa mara ya kwanza
Mungu ametupatia mbunge mwenye uchungu wa kweli na maendeleo yetu
hivyo lazima tumkumbatie azidi kutawala daima'
Akielezea
kuhusu miradi mbali mbali iliyofanyika katika kata yake alisema
kuwa awali umeme ulikuwepo mjini Ludewa pekee kwa kipindi chote
toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 na kuwa umeme huo aliuleta
aliyekuwa mbunge wao stanley kolimba ambae kwa sasa ni mwenyekiti
wa CCM wilaya ila kwa kipindi cha Filikunjombe vijiji zaidi
vimeendelea kupatiwa umeme na maendeleo mengine mengi ikiwemo
barabara ya lami Ludewa mjini.
Diwani
huyo aliwataka wananchi wa Ludewa kutoyumbishwa na wale wote wenye
uchu wa madaraka ambao wapo kwa maslahi yao na badala yake kubaki
njia kuu kwa kuendelea kuwa na mbunge Filikunjombe kwa kipindi
kingine zaidi.
'kwa
kuwa utaratibu wa chama ni kutangaza uchaguzi wa kura za maoni ila
kama ingeruhusiwa tungezuia chama kutoa fomu kwa wagombea wengine wa
ubunge ....lakini tunakuhakikishia wewe endelea kufanya maendeleo bila
hofu kwani ni mbunge wetu wa 2015-2020 na zaidi hadi mwenyewe
utakaposema basi sisi tupo na wewe'
Katibu
mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya alisema mbali ya
kubahatika kuwa katibu mwenezi wa mkoa wa Iringa uliokuwa na wilaya
zaidi ya 6 na majimbo zaidi ya 10 hakupata kuona mbunge anayejituma
kama Filikunjombe na kuwa mbali ya ubunge wake kuwanufaisha
wananchi wa Ludewa ila bado amefanikiwa kuutangaza mkoa wa Njombe na
kuwa moja kati ya wabunge wa mfano katika bunge.
Mgaya
alisema kama wabunge wote wa CCM wangeifanya kazi ya kuwatumikia
wananchi kama anavyofanya mbunge huyo wa Ludewa uwezekano wa
wapinzani kwenda bungeni ungekuwa mdogo zaidi na kuwa chuki ya
wananchi dhidi ya CCM ni kutokana na baadhi ya wabunge ,madiwani na
viongozi wengine wa umma kushindwa kuwajibika katika kuwatumikia
wananchi .
Nae
mbunge Filikunjombe akiwashukuru wananchi hao alisema kuwa moja kati
ya ndoto yake ni kuona wananchi wa Ludewa wanaungana na watanzania
wengine katika kunufaika na uhuru wao kwa kupatiwa umeme na huduma
nyingine za kijamii.
Kwani
alisema amepata kupigania kuona wananchi wa vijiji 14 vya jimbo la
Ludewa ambao walikuwa gizani kwa muda wote wa nchi ilipopata uhuru
wanapatiwa umeme kabla ya kumaliza kipindi chake cha kwanza na ubunge
na kuwa kamwe hatakubali kuona mtu yeyote anashiriki kukwamisha ndoto
yake hiyo ya kuwaletea maendeleo wananchi .
No comments:
Post a Comment