Wednesday, April 29, 2015

SHINDANO LA MAMA SHUJAA LAZINDULIWA WILAYANI KISARAWE


Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh.Subira Mgalu amezindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na kumkwamua kiuchumi.

Subira ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kumwezesha mwanamke katika kilimo na kumkwa mwanamke kiuchumi iliyofanyika  katika kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Subira amesema kufanyika kwa mashindano wilayani kwake ni fursa kwa wanawake kushiriki  kuchukua fomu za ushiriki na kuacha uvivu  na kutaka zawadi ya mshindi wa kwanza itokee wilyani humo.

 Aliongeza kuwa shindano hilo linawapa mwanamke uwezo wa kutambua haki zao umiliki wa ardhi na kuwa na ubunifu wa kuweza kubadilisha mbinu za kisasa za kilimo bora.

Nae Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona amesema  kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa wenyeji wa shindano hivyo wanawake wa kisarawe wanahitaji kujituma katika kuchangamkia fursa hiyo.


Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya fursa ambazo watazipata kupitia Shindano la  Mama Shujaa wa Chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu  akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo wakati uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
  Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam,Eluka Kibona akielezea Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
 Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akizungumza na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.
 Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengine pindi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula litakapoanza.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kwa kuleta Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Kijijini kwake.
  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akifurahi kwa Burudani ya Muziki pamoja na wananchi baada ya uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kijijini Kisanga.
  Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua Mama kiuchumi.
  Mh. Subira Mgalu akifurahi pamoja na Baadhi ya kinamama wa kijiji cha kisanga Baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.

 Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu za kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wananchi wa Kisarawe wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo wakto akizindua shindano la Mama Shujaa lililofanyika leo katika Kijiji cha Kisanga wilayani humo.

No comments:

Post a Comment