Wednesday, April 29, 2015

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA, APOKEA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 50 KUTOKA KAMPUNI YA TSN NA MIPIRA 50 KUTOKA KAMPUNI YA SMART SPORTS KWA AJILI YA MASHINDANO YA KINONDONI CUP

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kutoka Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) wa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yatakayoanza Juni 2015 katika wilaya hiyo.
 Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  Kinachosambazwa na Kampuni ya TSN, Khamis Tembo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda, akizungumza katika mkutano huo baada ya kutoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
  Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo (wa pili kulia), akimkabidhi jezi na vifaa vya michezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yaliyoanzishwa na Makonda. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN , Koiya Kibanga.
Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo akimvalishe moja ya jezi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya mashindano hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kushoto), akimkabidhi DC Makonda mpira mmoja kati ya 50 aliyoitoa kwa ajili ya mashindani hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN ambayo imetoa msaada wa vifaa hivyo vya michezo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo,Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN Group, Koiya Kibanga, Meneja Masoko na Mauzo wa TSN, Nafsa Soud na Mshauri wa TSN, Francis Bonda 'Kaka Bonda'
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kulia), ambaye ametoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiangalia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya TSN pamoja na Kampuni ya Smart Sports  ambayo imetoa mipira 50 kupitia Mkurugenzi wake, George Wakuganda.

 Suleiman Msuya

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea msaada wa jezi seti 100 na mipira 50 kutoka kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya mashindano ya mpira wa netibali na mpira wa miguu yatakayoitwa Kinondano Cup.

Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondani, Paul Makonda alisema mikakati yake ni kuhakikisha kuwa vijana wa Wilaya hiyo wanatumia vipaji vyao kujikwamua katika umaskini.

Makonda alisema mashindano hayo yatakuwa ni mpira wa miguu wanaume na wanawake, mpira wa kikapu wanawake na wanaume na mpira wa netibali ambao ni wanawake pekee.

"Nimedhamiria kuhakikisha kuwa jamii inaondokana na dhana kuwa wakazi wa wilaya hiyo ni watumia madawa na uchangudoa na njia sahihi ni kuwahusisha vijana na kutumia vipaji vyao," alisema.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huyo Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy ambacho ndio wametoa mtaasa huo kupitia TSN, Khamis Tembo alisema msaada huo una lengo la kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Tembo alisema kampuni ya TSN inatambua umuhimu wa michezo hivyo kupitia Chilly Willy wameona ni muhimu kutoa msaada huo wa jezi seti 100 na mipira 50 ili kufanikisha malengo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Smart Sport, George Wakuganda ambaye kampuni yake imetoa mipira 50 alisema wameamua kuungana na Mkuu wa Wilaya kwani wao ni wanamichezo.

Wakuganda alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Mkuu huyo wa Wilaya kwani jitihada zake za kuhakikisha vijana wanatoka katika dibwi la umaskini ni za maana.
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

No comments:

Post a Comment