Wednesday, April 22, 2015

Miradi inayokopesheka chanzo cha kupata Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana – Riwa

Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa katikati akizungumza na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli Bibi. Rose Mhina kulia kabla ya kukutana na vijana wa Kata ya Monduli juu na Kata ya Mfereji kutoa elimu ya ujasiriamali na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika Halmashauri ya Monduli Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa akitoa mada ya Ujasiriamali, Ujuzi na Stadi za Maisha kwa vijana wa Kata ya Monduli juu na Kata ya Mfereji leo katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwaelekeza vijana walioudhuria semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka kata za Monduli juu na Mfereji Halmashauri ya Wilaya ya Monduli jinsi wanavyotakiwa kuzingatia mwongozo unaosimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada ya Uongozi bora wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika Kata ya Monduli juu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Afisa Ushirika kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Ester Tarimo akiteta na vijana wa kata ya Monduli juu na Mfereji namna ya kujiunga na Saccoss kwa maendeleo ya vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika Kata ya Monduli juu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Vijana wa Kata za Monduli juu na Mfereji wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika Kata ya Monduli juu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Mmoja wa washiriki wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana akichangia wakati wa semina hiyo iliyofanyika leo katika kata ya Monduli juu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Vijana wa Kata za Monduli juu na Mfereji katika picha ya pamoja na wahamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na wadau wa vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli baada ya kufunga semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Kata ya Monduli juu Halmashauri ya Monduli Mkoa wa Arusha. Picha na Genofeva Matemu – Maelezo Monduli.

Na: Genofeva Matemu – Maelezo Monduli

Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kata za Monduli juu na Mfereji wametakiwa kuwa na miradi ya mfano inayokopesheka na inayoonekana ili kuweza kupata fedha zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaosimamiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Rai hiyo imetolewa na Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika leo katika Kata ya Monduli juu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.

Bibi. Riwa amesema kuwa jitihada za awali zifanywe na vijana wenyewe kwa kuwa na mwamko wa kuleta maendeleo yatakayotokana na miradi endelevu na yenye malengo kwani kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na hali ya maisha ya sasa na kuwa mfano katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Aidha Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli Bibi. Rose Mhina amewataka vijana wa Monduli kutokupenda kubebwa kwa kupewa fedha za bure kwa kununuliwa na wanasiasa bali wazidi kujijengea mazoea ya kuwekeza na kuchukua mikopo inayotolewa na Serikali kwa vijana yenye riba nafuu na kurejesha fedha hizo kwa wakati ili vijana wengine waweze kufikiwa na fursa hiyo.

Akizungumza na vijana wakati wa semina hiyo Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Ester Tarimo amewataka vijana kutokuwa watu wakusukumwa kutafuta maendeleo yao bali wawajibike na kutafuta fursa zilizopo ili kuweza kuondokana na hali ya kutegemea kazi moja ya ufugaji wa mifugo.

“Vijana wa Munduli hamjazaliwa kuishia hapo mlipo, msipende kusukumwa na watu kutafuta maendeleo yenu changamkieni fursa zilizopo na kuwajibika katika jamii zenu bila ya kuwa na ubaguzi wa kijinsia kwani Monduli haitakiwi kuwa kama ilivyo kwa sasa” alisema Bi. Tarimo.


Kwa upande wake mshiriki wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana Bw. Mboyo Kayai amesema kuwa vijana wa Monduli wanaweza kama watapatiwa elimu ya watu wazima kwani kwa sasa jamii kubwa ya vijana katika Halmashauri hiyo hawajui kusoma na kuandika kitu kinachowapelekea kushindwa kuwa na mbinu mbadala za kiujasiriamali.

No comments:

Post a Comment