Thursday, April 23, 2015

MANISPAA YA ILALA YAELEZEA UBORESHAJI WA UKUSANYAJI WA MAPATO YAKE

Meneja Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri hiyo. Kulia ni Meneja Kodi Majengo, Stellah Mgumia.
 Meneja Kodi Majengo wa Manispaa hiyo, Stellah Mgumia akitoa ufafanuzi mbalimbali wa ukusanyaji wa mapato.
 Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa Manispaa hiyo, Francis Luambano (kushoto), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
 Ofisa Biashara wa Manispaa hiyo, Dennis Mrema, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MANISPAA ya Ilala imewaonya wafanya biashara wanaotumia madalali kulipia huduma zinazopatikana katika manispaa hiyo waache maana wamekuwa chanzo cha upoteaji wa mapato katika manispaa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Meneja Uhusiano wa Manispaa hiyo Tabu Shaibu  alisema uboreshaji wa mapato unategemea sana uaminifu wa walipa kodi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyotegemewa katika manispaa hiyo.

"Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inategemea mapato yake kutoka kwa wafanya biashara na wamiliki wa nyumba waaminifu wanaolipa kodi kwa wakati ili kutekeleza shughuli za maendeleo".

Shaibu alisema manispaa inategemea vyanzo vinne vya mapato ambavyo ni kodi ya majengo, leseni za Biashara, ushuru wa mabango na kodi ya huduma za jiji.

Kodi nyingi imeishia mikononi mwa watu wanaojiita madalali au vishoka sababu ya kukosa uaminifu kwa wale waliowatuma na kuingiza waliowatuma katika hatia ya ukwepaji kodi, aliongeza Shaibu.

"Walipa kodi wengi wamejikuta hatiani baada ya kuwatumia madalali au vishoka wasio waaminifu kulipa kodi na kujikuta stakabadhi zao hazipo katika kumbukumbu ya stakabadhi za manispaa za walipa kodi na kusababisha walipe faini mara tatu ya kodi au kushtakiwa mahakamani kwa kosa la kughushi".

Shaibu alielezea zoezi la tathmini ya majengo ya biashara na makazi linaliendelea katika manispaa hiyo ili kujipanga ma ukusanyaji wa kodi wa mwaka wa fedha 2015/16 unaoanza tarehe mosi julai.

"Tunaomba ishirikiano kutoka kwa wakazi wa wilaya ya Ilala ili tuweze kupata makadirio ya kodi ya kodi ya majengo ambayo ni asilimia 0.15 kwa jengo la makazi na asilimia 0.20 kwa jengo la biashara".


Shaibu ametoa wito kwa walipa kodi kuhakikisha wanalipa kodi kwenye mamlaka husika na kama walishatumia madalali au vishoka wakahakiki nyaraka zao manispaa ili wasije kuingia matatizoni." 

(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/

No comments:

Post a Comment