Friday, April 10, 2015

FILIKUNJOMBE AKABIDHI MSAADA WENYE THAMAMANI YA ZAIDI YA TSH MILIONI 32 HOSPITALI YA WILAYA YA LUDEWA

Mbunge  wa   jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  kulia  akikabidhi msaada wa  mataulo na mito kwa  mkurugenzi  wa  Halmashauri ya  wilaya ya  Ludewa  Wiliam Waziri kwa  ajili ya  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa.
Filikunjombe  mwenye  T-Shet ya  CCM  akisaidiana na  watumishi wa  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa  kushusha  vifaa mbali mbali.
Watumishi wa  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa  wakimshangilia mbunge  wao  Deo Filikunjombe kwa msaada Hospitalini hapo
Mbunge  wa  Ludewa  akizungumza na  watumishi wa Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa.
Watumishi wa  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa  wakimshangilia mbunge  wao  Deo Filikunjombe kwa msaada Hospitalini hapo
Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akionyesha   mataulo ya  kisasa

Watumishi  wa Ludewa  Hospitali  wakimsikiliza mbunge  wao
Katibu  mwenezi wa  CCM mkoa  wa  Njombe  Honoratus  Mgaya  kulia  akimtazama mbunge  Filikunjombe  wakati  akisisitiza uwajibikaji mzuri kwa  watumishi wa Hospitali ya  wilaya ya Ludewa  kushoto ni mkurugenzi wa Halmashauri ya  Ludewa  Wiliam waziri
mbunge wa  Ludewa  Deo Filikunjombe  kushoto akishiriki  kushusha  shehena na  vifaa mbali mbali  alivyovitoa katika  Hospitali ya wilaya ya  Ludewa
Filikunjombe  mwenye  T-Shet ya  CCM  akisaidiana na  watumishi wa  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa  kushusha  vifaa mbali mbali
Mbunge  wa  Ludewa Deo Filikunjombe  mwenye  T-Shet ya  CCM  kulia  akisaidiana na  watumishi wa  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa  kushusha  vifaa mbali mbali
Katibu  mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe  Honoratus  Mgaya  wa  tatu  kushoto  akisaidia  kushusha mizigo
Vitu  vilivyotolewa na  Filikunjombe
Mbunge  Filikunjombe  akifurahi  jambo  wakati  akizungumza na   watumishi wa  Hospitali  ya  Ludewa mara  baada ya kukabidhi misaada  mbali  mbali 
Moja kati ya  magari ya  wagonjwa  yaliyotolewa na mbunge wa  Ludewa  Deo  Filikunjombe  jimboni mwake  kusaidia kubeba  wagonjwa  
                                       Na FG Blog, Ludewa

KATIKA kukabiliana na tatizo la uhaba wa vifaa mbali mbali katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe mbunge wa Jimbo la Ludewa (CCM) Deo Filikunjombeamekabidhi msaada wa Mashuka ya wagonjwa 200, Blanketi ya kisasa 100,taulo za kuogea wagonjwa 200 pamoja na mito 100 ya kulalia wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 32 .

 Mbunge huyo amefikia hatua hiyo kutokana na tatizo kubwa la Hospitali hiyo kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo na vifaa hivyo kwa wagonjwa .

 Akikabidhi msaada huo hospitalini hapo jana mara baada ya kuzungumza na watumishi wa sekta ya afya Mbunge huyo ,aliwataka watumishi hao kuwa waaminifu kwa kuviangalia vifaa hivyo visipotee na badala yake wavitunze na vitumike kwa ajili ya wagonjwa na si vinginevyo .

 Alisema,anathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na watumishi hao katika kuwahudumia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo lakini amewataka kuthamini wapiga kura wake hao kwa kuwapatia huduma inayostahiri na kuokoa maisha yao.

 “Nawaomba sana ndugu zangu watumishi mjitahidi kutunza hivi vifaa nilivyoleta ilimnitie moyo niendelee kusaidia zaidi ,kwani hii ni fedha yangu binafsi niliyokaata kwenye posho yangu ya vikao vya bunge pia naomba muithamini sana kazi yenu ,kwani ajira ni ngumu na kuna watu wanahangaika huko mitaani kutafuta ajira pamoja na usomi wao hakuna ajira, tuwatumikie wagonjwa kwa upendo na furaha ikiwa ni pamoja na kuhokoa maisha yao kwani wanachohitaji toka kwenu ni upendo na huduma nzuri tu,alisema Filikunjombe.

 Awali akisoma Risala fupi ya hospitali hiyo kwa Mbunge huyo Kaimu Mganga mkuu Hospitali ya Wilaya ya Ludewa Apolnary Nombo alisema,

Watumishi hao wanaheshimu jitihada kubwa ambazo amezifanyahususani kwenye sekta hiyo katika kipindi cha miaka mitano ainaonekana na zinapimika ndani na nje ya Bunge ikiwa ni pamoja na kuwatembelea mara kwa mara na kutoa misaada hospitalini hapo.

  Hata  hivyo  alisema  bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo zinakwamisha maelengo yao ikiwemo ya kukosekana vifaa muhimu katika jengo la upasuaji ikiwemo mashine ya kuchemshia vifaa vya upasuaji na mashine za kutolea dawa za usingizi .

 Pia  changamoto nyingine ni uchakavu wa jengo la wazazi ambao unapingana na MDG 4 na 6 upunguzaji wa vifo vya wazazi pamoja na ukosefu wa chumba cha watoto wachanga ambao wakizaliwa njiti wanahitaji  huduma   hiyo  pamoja na changamoto  nyingine  ambazo  waliomba msaada  wa mbunge   huyo .

Mganga  huyo  alipongeza   jitihahada  mbali mbali  ambazo  zimekuwa  wakifanywa na  mbunge  Filikunjombe  katika  Hospitali  hiyo na Zahanati  za vijiji  mbali mbali katika  wilaya ya  Ludewa na kuwa  pasipo  kuboresha  huduma  za afya  kwenye  zahanati hizo  yawezekana  idadi ya  wagonjwa  kukimbilia katika  Hospitali  hiyo ya  wilaya  ingekuwa  kubwa  zaidi.

No comments:

Post a Comment