Monday, April 6, 2015

FILIKUNJOMBE AIPONGEZA NEC ASEMA JK ATAKUMBUKWA DAIMA NA WATANZANIA

mbunge  wa  jimbo la  ludewa Deo Filikunjombe akishiriki ibada ya pasaka na  waumini wa kanisa  la RC MAVANGA
MBUNGE WA  LUDEWA  DEO FILIKUNJOMBE AKITOA SALAM ZA PASAKA KWA  WAUMINI WA KANISA LA RC MAVANGA
PAROKO WA MAVANGA AKIMKABIDHI MBUNGE FILIKUNJMBE  ZAWADI YA  KUKU BAADA YA MBUNGE  HUYO  KUTOA ZAWADI  MBALI MBALI KATIKA MAKANISA YA LUDEWA ZIKIWEMO BATI 300 NA VITI
WAUMINI  WA MAVANGA WAKIMKABIDHI MBUNGE FILIKUNJOMBE KUSHOTO NDIZI
MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJ0MBE KATIKATI   AKIWAELEKEZA JAMBO  WAUMINI  JAMBO
WAUMINI MAVANGA  WAKIMPONGEZA MBUNGE FILIKUNJOMBE KWA MISAADA  YAKE
MZEE  WA KANISA LA KKKT LUDEWA MJINI AKIWA AMEBEBA  KINANDA KILICHOTOLEWA NA MBUNGE  DEO FILIKUNJOMBE
VIONGOZI WA KKKT  LUDEWA  MJINI  WAKIONYESHA VIFAA VYA MSAADA  TOKA KWA  MBUNGE
WAUMINI  KKKT WAKISHIRIKI UBATIZO
DIWANI  WA KATA YA MLANGALI FARAJA MLELWA AKISHIRIKI  KUBATIZA MTOTO  WAKE
WAUMINI KKKT  LUDEWA  MJINI  WAKIWA KATIKA IBADA YA PASAKA
NA MatukioDaima Blog
MBUNGE wa   Ludewa  Deo Filikunjombe aipongeza  tume ya taifa  ya uchaguzi (NEC) Kwa kusogeza  mbele zoezi la upigaji kura  za maoni kwa katiba inayopendekezwa na  kuwa  hatua iliyofikiwa katika mchakato  huo ni kubwa na kumbukumbu kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete anapoondoka madakarani na urithi kwa Rais ajaye kuendeleza mchakato  huo.

Filikunjombe  alitoa pongezi  hizo wakati akitoa salamu  zake za pasaka jana kwa waumini  wa madhehebu mbali mbali ya  Kikristo  katika  wilaya  ya  Ludewa   salam zilizoambatana na msaada  wa  viti  ,bati ,vinada  na saruji katika makanisa   hayo kama moja  ya utekelezaji  wa ahadi  zake kwa  madhehebu  hayo kama ambavyo  walivyomuomba .

Alisema  kuwa hatua  ya tume  ya taifa ya  uchaguzi  kuongeza  muda katika zoezi hilo la kura  za  maoni kwa  katiba inayopendekezwa mbali yakuwapunguzia majukumu  watanzania ya kufanya mambo  mengi kwa wakati mmoja bado kusogezwa  huko  mbele kutawafanya watanzania hasa wananchi  wake  wa ludewa kuendelea na shughuli  nyingine  za uzalishaji mali.

'hakuna uharaka  wa  kuharakisha  zoezi la  upigaji kura za maoni katika katiba  inayopendekezwa kwani hadi  sasa hatua iliyofikiwa ni  nzuri na kumbukumbu  kubwa kwa rais Jakaya kikwete anapomaliza  muda  wake kuwa amefanya jambo  hilo  kubwa hadi lilipoishia na Rais ajaye ataanzia alipoishia kikwete kwa kukamilisha katiba   hiyo  kuliko kukimbizana kama ilivyopangwa awali kabla ya tume kusogeza  mbele  zoezi hilo kwa  muda usiofahamika'


pia mbunge  huyo  aliwataka  vijana kuwa  wazalendo na nchi  yao  badala ya kukubali kutumika na baadhi ya watu  wasioitakia mema  nchi  na kuwa hatari ya  vijana kutumika ni mwanzo  wa nchi  kuja  kuingia katika machafuko kama zilivyonchi nyingine ambazo  kila uchwao ni machafuko  na chimbuko ni vijana wao  kukosa  uzalendo .

Hata hivyo alisema kuwa  wakati Taifa  likijiandaa kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi octoba mwaka  huu kuna matukio makubwa  ya  kitaifa yanayoendelea likiwemo la kujiandikisha kwenye  daftari la  kudumu la wapiga  kura na kuwa  ni kipimo kwa watanzania hasa  vijana  kuanza  kuonyesha uzalendo kwa kuwa  waaminifu katika zoezi hilo badala  ya  kutumiwa na baadhi ya watu  wanaotaka uongozi kwa kupitia njia za  panya kwa maana ya  kuwaandaa vikundi  vya  vijana kujiandikisha zaidi ya mara  moja katika  vituo  tofauti jambo ambalo ni hatari katika nchi na kufanya   hivyo  ni kosa la jinai kisheria.

Huku akiwaonya vijana kuepuka  kufanya udanganyifu  wa  kujiandikisha mara  mbili katika daftari la kudumu la wapiga kura zoezi  linaloendelea na kuwa hadi  sasa kata  ya  mlangali ludewa   kuna kijana mmoja ambae  anashikiliwa na polisi kwa tuhuma  za kujiandikisha zaidi ya mara moja

Filikunjombe  amewataka  waumini  wa  dini  ya  kikristo wilayani Ludewani  mkoani  Njombe kusherekea  sikukuu ya  kufufuka  kwa Yesu kristo  kwa  kuendelea  kuliombea  Taifa  kuondokanana mabalaa mbali mbali  kwa  mwaka  huu  tunapoelekea  kuingia katika  uchaguzi  mkuu Octoba  

Wakati  waumini  wa kikristo  hapa  nchini jana  wakiungana na  waumini wenzao  ulimwenguni kusherekea kumbukumbu ya  kufufuka kwa  Yesu  Kristo sikukuu ya pasaka  makanisa wilayani  Ludewa mkoani  Njombe  yakitumia sikukuu  hiyo  kuhimiza  waumini  wao  kuepuka  kujiungiza katika makundi  ya kuvuruga amani ya  nchi  katika  kipindi hiki  cha  kuelekea katika  uchaguzi mkuu .

Makanisa  hayo yalitoa kauli  hiyo  baada  ya  kusoma  wakara  wa amani  wa salam  za Pasaka  uliosambazwa katika makanisa  yote na mbunge  wa  jimbo  la  Ludewa  Deo Filikunjombe .

Mchungaji  wa Kanisa   la  Kiinjili la  Kilutheri  Tanzania (KKKT)  Tafuteni Mwasonya  wakati  akitoa  salam za  pasaka  na  kumshukuru  mbunge wa Ludewa  Deo  Filikunjombe  kwa msaada  wa viti  100 vya  Plastiki na kinanda   kanisani hapo .

Alisema  kuwa  kwa upande  wake  hajapata  kukutana ana  kwa ana na mbunge  Filikunjombe  toka  alipochangulia   ila amekuwa  akukutana  na shughuli mbali mbali  za kimaendeleo  ambazo  zimefanywa na mbunge  huyo  na  kushuhudia utendaji kazi  wake  mkubwa katika  jimbo  hilo.

Hivyo  alisema  wana  nchi  wa  Ludewa wana  kila  sababu ya  kujivunia  kwa  kuwa na mbunge kama  huyo na  kama  ingekuwa  inaruhusiwa ndani ya kanisa  kuweka picha  ya  kiongozi wa  wananchi basi angeweka  bango  maalum  ambalo  limetolewa na mbunge  Filikunjombe la  kuwakumbusha  wananchi  wa  Ludewa  orodha ya  wabunge waliopata  kuongoza  jimbo  hilo hadi mwaka  huu 2015 .

“ Kwa  utaratibu  wetu  wa  kanisa la Kirutheri  ndani ya kanisa   tunaweka  picha  ya  Yesu Kristo  pekee hata  picha  ya  askofu  wetu  hatuweki  ila  kama  ingekuwa  inaruhusiwa  kuweka  picha  za  zaidi  kanisani basi  tungeweka  picha ya  orodha ya  wabunge  wetu  lakini  haturuhusiwi  kufanya  hivyo  ……lakini  orodha   hiyo ya  wabunge  mheshimiwa  Filikunjombe  ametuandalia na  kila mmoja atapewa na ruksa  kwenda  kuweka  nyumbani kwake “ alisema mchungaji  huyo.

Hata  hivyo  alisema sherehe ya  kuviombea  vitu   hivyo  vilivyotolewa na mbunge  Filikunjombe na kumwombea  mbunge  huyo  ili azidi  kupata baraka  zaidi ya  kuongoza  Ludewa wanapanga  kuifanya  wakati  wowote   baada ya  sikukuu  za Pasaka na kuwa  siku  hiyo watamwalika  na mbunge  ili  waweze  kumbariki  pia.

Pia  mchungaji huyo  aliwataka  waumini  wa  kanisa  hilo  kujiepusha na ushiriki  wa  vurugu  zisizo na msingi katika  taifa  letu  hasa  wakati  huu wa  kuelekea katika  uchaguzi mkuu  na  badala  yake  kujikita  zaidi katika  maombi  kwa  Taifa  ili nchi  izidi  kubarikiwa kwa amani  na utulivu.
Huku Paroko ya Parokia ya Ludewa mjini  Padre Cathbert  Mlowe, alisema licha ya kuwa muumini katika kanisa hilo, mbunge huyo amekuwa na kasumba ya kuwasaidia watu bila kujali tofauti za imani na itikadi zao.

“Ninajua ninaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti, lakini nitasema tu ya kwamba Filikunjombe amekuwa mfano wa viongozi wanaowakumbuka wahitaji kwa nyakati zote, na amekuwa mtu wa kurejea kwetu (Ludewa) mara kwa mara, viongozi wa aina hii ndio wanaopaswa kushikwa mkono,”
Alisema wakati ambapo taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, wapo watu watakaijitokeza na kujinasibu kwa namna tofauti, ikiwa ni pamoja na kukumbushia udugu uliopo kati yao na jamii za mahali wanapotoka ili wachaguliwe.
“Watu wanaojitokeza kwenye jumuiya zetu na kujitambulisha kwa familia na ukoo wanazotoka ili wachaguliwe, hawapaswi kupata nafasi hizo. Tujiandaye kuwachagua viongozi wanaotokana na sisi, wale wanaokumbuka na kurudi kuungana nasi katika kukabiliana na changamoto zetu kama anavyofanya huyu mwenzetu,” alisema.

Kwa  upande  wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Anatoly Chowa, alitumia misa hiyo kujitambulisha kutokana na kuhamishiwa wilayani humo akitokea wilayani  Mbulu mkoani Manyara.

Chowa alisema Filikunjombe ni mbunge anayewatumikia wananchi kwa ubunifu unaokidhi mahitaji ya umma, hali iliyo tofauti na wawakilishi wengine.

Chowa aliyewahi kuwa Mbunge wa Biharamuro kwa miaka 10, alisema katika kipindi chote cha ubunge wake hakuwahi kuwasaidia wapiga kura wake kama anavyofanya Filikunjombe.

“Nimekuwa Mbunge kwa miaka 10, nimehudumu na Horace Kolimbe (maremu), Stanley Haule na Stanley Kolimba, sijawahi kuyafanya mambo ama kuwasikia wenzangu hao wakiyafanya kama anavyofanya Filikunjombe,” alisema.

Huku  paroko wa  RC  Lupingu   Chrisantus  Mlelwa  mbali ya  kumshukuru  mbunge  Filikunjombe kwa   salam  zake za pasaka  kwa  waumini  wa kanisa  hilo bado  alipongeza msaada  wa  kinanda  kilichotolewa na mbunge  huyo  huku  akiwataka  waumini  wa  kanisa  hilo  kuzidi  kuliombea  Taifa na  kumwombea  mbunge  wao  huyo

No comments:

Post a Comment