Sunday, April 19, 2015

BENKI YA CBA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 5 KWAAJILI YA UJENZI WA HOSTELI YA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI KIFARU MWANGA

SAM_2053
Meneja masoko wa benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe kushoto,Meneja masoko Moshi Eliud Marko katikati wakimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika kijiji cha kituri kata ya kileo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro hundi ya shilingi Milioni tano yenye thamani ya zaidi ya mifuko 300 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika shule hiyo ,msaada huo ni sehemu ya kamapeni ya Book by Book inayoendeshwa na benki ya CBA ikilenga kusaidia serikali katika juhudi za Elimu(Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)
SAM_2042
Meneja masoko wa Benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe akizungumza na wanafunzi(hawapo pichani) kuhusu nia yao ya kuwasaidia msaada huo wa saruji kwaajili ya kujenga hosteli ni kutokana na idadi ya wanafunzi 944 kuwa na changamoto kubwa ya ufaulu hasa jinsia ya kike huku akiwaasa wanafunzi hao kuwa Elimu ndio urithi pekee wa kuweza kuharakisha maendeleo Tanzania hivyo jamii inategemea kupata watu muhimu wakuwasaidia kama madaktari,wafanyakazi wa mabenki na hata walimu wa kuendeleza elimu
SAM_2038
Meneja masoko Moshi Eliud Marko akiwa anasisitiza wadau mbalimbali wa makampuni makubwa kujitokeza kusaidia kuinua Elimu ili kupunguza umaskini Nchini
SAM_2033
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro akiwa anatoa neno lake la  shukrani kwa Benki ya CBA kwa kufika na kuguswa kusaidia hosteli ya wasichana katika shule hiyo kutokana na wengi wameshindwa kuendelea na masomo shuleni baada ya kuingizwa katika mahusiano na wanaume hali ambayo inawawia vingumu kuweza kumudu masomo.
SAM_2060
Mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule hiyo  Neema  Emmanuel akitoa neno la shukrani

SAM_2050
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Kifaru wakiwa wanasikiliza kwa makini
SAM_2061
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa msaada huo alisema Msaada huo utakuwa kichocheo kwa wanafunzi wa kike kufanya vizuri zaidi ambapo shilingi Milioni 64 zinahitajika kukamilisha hosteli hiyo itakayoweza kuhudumia wanafunzi 80

SAM_2064
Picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa KeyMedia Agency Limited Bi Barbra Lazaro
SAM_2065
Mafundi wakiwa wanaendelea na ujenzi wa hosteli ya wasichana shule ya kifaru
SAM_2066
Ugeni kutoka Benki ya CBA wakiwa wanashuhudia eneo la ujenzi wa hosteli wakiongozwa na mwalimu Mkuu wa shule hiyo

SAM_2067
Kazi inaendelea
SAM_2068
Mifuko ya Saruji

No comments:

Post a Comment