Friday, March 6, 2015

TTCL yatoa Msaada wa Madawati kwa Shule ya Msingi Bunena,Bukoba

Uongozi wa TTCL ukitoa Msaada wa Madawati katika Shule yaShule ya Msingi  Bunena leo Ijumaa.TTCL inaamini kutoa msaada huo wa Madawati utasaidia kuboresha Ufanisi wa Shule na hatimaye kupata Matokeo Makubwa sasa katika Sekta ya Elimu. Pia ni Mategemeo ya TTCL kuwa utaleta chachu kwa wadau wengine katika Sekta kuweza kuchangia katika sekta hiyo pana ya Elimu. Hatimae kuondoa Changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu hapa Mkoani Kagera na Nchi nzima kiujumla. TTCL pia imeweza kuwahakikishia wadau mbalimbali waliohudhuria hafra hiyo kuwa wataendelea kuwa bega kwa bega katika kuleta maendeleo kadri hali ya kifedha itakavyoruhusu.
Wanafunzi wakikalia dawati moja wapo ambapo dawati moja litakaliwa na Wanafunzi 3 hivyo madawati hayo yatawatosha wanafunzi 150 wa Shule hiyo ya Bunena. Picha na Faustine Ruta, BukobaBaadhi ya Viongozi wakishukuru kwa Zawadi hiyo ya Madawati.
Wanafunzi wakisoma Risala mbele ya Viongozi waliohudhuria hafra hiyo katika shule ya Msingi Bunena wakati wa Kukabidhi Msaada wa Madawati.
Risala ikikabidhiwa kwa mgeni Rasmi Meneja wa TTCL Mkoa wa Kagera Bw. Salum Mbaya(kulia).
Kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu (TTCL) leo Kampuni hiyo imekabidhi Madawati 50 yenye thamani ya Tsh 2.5 Milioni. Kila Dawati lina uwezo watoto 3 hivyo watoto 150 wataweza kukaa katka Madawati hayo. Msaada huo ikiwa ni kuitikia Wito wa kuchangia Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Kagera na hatimae Taifa zima. Picha na Na Faustine Ruta, Bukoba
Mkuu wa Wilaya akitoa neno
Wanafunzi wa Shule hiyo iliyopo Bukoba eneo la Bunena na shule ikijulikana Bunena Shule ya Msingi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa TTCL kwa furaha wakisikiliza neno kutoka kwa Mgeni Rasmi

Meneja wa TTCL Mkoa wa Kagera Bw. Salum Mbaya
Wanafunzi wa Shule hiyo wakiimba Nyimbo
Meneja wa TTCL Mkoa wa Kagera Bw. Salum Mbaya na (kushoto) ni Bw. Steven Msumali
Picha ya pamoja ilipigwa.

No comments:

Post a Comment