Sunday, March 29, 2015

TAIFA STARS YATOSHANA NGUVU NA MALAWI, JIJINI MWANZA LEO

Viongozi mbali mbali pamoja na Timu zote mbili wakiwa wamesimama kwa dakika chache kumkmbuka Kiongozi wa mpira wa Miguu, Aliyetangulia mbele ya haki, Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa Star, Marehemu Sylvester Marsh aliyefariki dunia hivi karibuni katika Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Mjini Mwanza.PICHA ZOTE NA FAUSTINE RUTA WA BUKOBA SPORTS.
Viongozi mbalimbali waliojitokeza katika Mpambano huo wa Taifa Stars na Malawi CCM Kirumba Jijini Mwanza leo Jumapili tarehe 28.03.2015
Wimbo wa Taifa uliimbwa kabla ya Mechi kuanza, (Picha na Faustine Ruta)
Timu zote mbili kwenye mstari tayari kwa kuanza kipute
Kikosi cha Malawi baada Wimbo wao wa Taifa kumalizika kuimbwa
Kikosi cha Taifa Stars kikiimba wimbo wa Taifa
Viongozi wakisalimia Mashabiki walioingia kwa Wingi Uwanjani hapo CCM Kirumba, Picha na Faustne Ruta
Timu zikisalimiana
Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza
Waamuzi wa Mtanage
Kikosi cha Malawi
Tayari kwa mpambano kuanza..
Shilingi kutafuta uelekeo
Picha ya PamojaBao 1-0 dakika ya tatu tu Malawi walipata bao kupitia kwa Esau Kanyenda baada ya mapeki wa Stars kujichanganya
Wachezaji wa Malawi wakipongezana baada ya kupata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa Esau Kanyenda kwa kufanya 1-0
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa "Taifa Stars", Thomas Ulimwengu akitafuna namna za kuuchukua mpira uliomilikiwa na Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Malawi wakati wa mtanange wao uliopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanzawa. Mchezo huoulimalizika kwa kufungana bao 1 -1Beki wa Taifa Stars, Shomari Kapombe akionyeshana uwezo wa kutunishiana misuli na Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Malawi wakati wa mtanange wao uliopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanzawa. Mchezo huoulimalizika kwa kufungana bao 1 -1.
Taifa Stars 0-1 Malawi dakika ya 3 mapema Malawi walishachafua ubao
Kipa wa Malawi akiondosha mpira langoni mwake
Pisha!
Fundi!
Kipa wa Malawi akiondosha mpira kwa kuupangua kutoka eneo la hatari
Mashabiki waliingia kwa wingi leo CCM Kirumba
Mashabiki jukwaa kuu
Meza Kuu Rais wa Tff Bw. Jamal Malinzi nae alikuwepo kushuhudia kipute!
Nyomi
Katikati ni Bw. Abdrazack kutoka Mjini Bukoba/Kasibante 88.5 FM Radio akitangaza live mpira huo kutoka CCM Kirumba Jijini Mwanza
Mashabiki waliingia kwa wingi
Mpaka mapumziko Stars ilikuwa nyuma ya 1-0
Waamuzi wakitoka kwenda kupumzika wakati wa mapumziko dakika chache
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Stars Mart Nooij akiteta jambo na Kiongozi wa soka wakati wa mapumziko baada ya dakika 45 kupita, wakiteta jinsi ya kupangua na kuweza kusawazisha na hatimae ushindi!!
Kipindi cha pili tunafanyaje??? Ngassa aingie au??
Muuaji wa bao la Malawi Essau kanyenda wakati wa mapumziko
Yale yale Ngassa na wenzake wakitoka Uwanjani kwenda kujumuika na kusikia neno kutoka kwa kocha mkuu Mart Nooij nini kinafanyika kipindi cha pili.
Patashika kwenye lango la Malawi kipindi cha pili
Mbwana Ally Samatta akishangilia bao baada ya kuisawazishia bao Taifa Stars kwa kufanya 1-1 dakika ya 76 kipindi cha pili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza leo hii, Picha na Faustine Ruta
Asante baba!! Samatta akipongezwa
Shabiki akifanya mbwembwe zake baada ya Taifa Stars kusawazisha bao1-1
Samatta akipongezwa
Baadhi ya Wachezaji wa Taifa Stars nao walimpongeza Samatta
Wakirudi kati kuanzisha mpira
Pongezi kwa Samatta Ally Mbwana
Mashabiki
Wakishuhudia live Mtanange CCM Kirumba
Mtanange umemalizika dakika 90 kwa nguvu sawa 1-1
Waandishi wa Habari wakipata mahojiano moja kwa moja kutoka kwa Afisa habari wao Malawi akiwa sambamba na Baraka Kizuguto wa Tanzania kupitia Tff

No comments:

Post a Comment