Monday, March 2, 2015

Rais Kikwete aongoza maelfu ya waombolezaji kuaga mwili wa Kapteni John Komba

Jeneza lenye mwili wa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,Marehemu Kapteni John Komba likiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam,wakati wa shughuli ya kuaga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI NA EMMANUEL MASSAKA.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiifariji familia ya marehemu.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,Luteni Jenerali Samuel Ndomba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho akifuatana na Naibu IGP,Abdulrahman Kaniki.
 Kingunge Ngombale–Mwiru akitoa heshima za mwisho.
Kamanda Kova.
Baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wakiifariji familia ya Marehemu.
Mhe. Ole Sendeka akibubujikwa na machozi kuondokewa na Mbunge mwenzake.
Familia ya Marehemu.

Watoto wa Marehemu Kapteni John Komba wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu baba yao.
Mjane wa Marehemu,Kapteni John Komba,Mama Salome Komba akiaga mwili wa mumewe
Khadija Kopa.
Umati wa viongozi mbali mbali pamoja na wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,Mh. Saidi Mtanda akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Kamati yake.


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Mh. Joshua Nassari.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akitoa salamu za Chama.
Mh. Muhongo akitoka kuaga mwili wa Kapteni Komba.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akisungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana.kushoto ni Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.
Mama Regina Lowassa akizungumza jambo na Mama Asina Kawawa.
Mh. Mkapa akizungumza jambo na Mh. Anne Makinda.



Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Edward Lowassa

MC wa shughuli hiyo Bw. Saidi Yakub wa Bunge akiwa kazini
Mjane wa Marehemu.

































2 comments:

  1. May his soul rest in eternal peace, Amen. Tutakukumbuka sana Mhe. Capt. Komba kwa mchango wako mkubwa kwa Taifa. Binafsi, sitasahau sauti yako 'unique.' Ni pigo kubwa lakini hatuna jinsi. Bwana alitoa na ndiye amekutwaa urejee kwake. Jina lake lihimidiwe. Poleni sana wafiwa wote na wale wote walioguswa na msiba huu.

    ReplyDelete
  2. Bwana awe mfariji wenu wanafamilia katika majonzi haya makubwa.
    Tunamwombea marehemu Captain Komba Alazwe mahala pema katika ufalme wa Mbinguni.
    Tutakumbuka mchango wako mkubwa kwa nchi yetu pendevu. Tuombee huko ulikokwenda amani na utulivu vizidi kutawala katika nchi yetu.
    Apumzike kwa amani.

    ReplyDelete