Tuesday, March 3, 2015

MHE. JANET MBENE AKAMILISHA ZIARA YAKE UINGEREZA KWA KUKUTANISHWA NA WAFANYABIASHARA WA KITANZANIA JIJINI LONDON

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Tanzania, Mheshimiwa Janeth Mbene(kulia), akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Lord Clive Hollick, walipokutana kuzungumzia masuala ya Biashara ya kati ya nchi mbili ya Tanzania na Uingereza na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Uingereza kusaidia wawekezaji wa Kiingereza kuwekeza Tanzania.
 Mheshimiwa Janeth Mbene, akiongeza na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Kiingereza alipokutana nao kwa mwaliko wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa East African Association. Mheshimiwa Naibu Waziri alikutana na Wafanyabiashara hao kwa lengo la kuwashawishi kuja kuwekeza nchini Tanzania
 Mheshimiwa Waziri Janeth Mbene(kulia), alipokutana na Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza na Chama cha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchini Uingereza (UKTI) (kati mwa picha), kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania nchini Uingereza, Bwana Yusuf Kashangwa.
 Wawakilishi wa Jumuiya za Wafanyabiashara na Wanachama wa chama cha Wafanyabiashara wa Tanzania nchini Uingereza (Tanzania Business Group) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda, Mheshimiwa Janeth Mbene, alipokutana na kuzungumza nao siku ya Ijumaa tarehe 28 Februari 2015, mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London. Mheshimiwa Waziri alikutana nao kuzungumzia hali ya Siasa na Uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Mheshimiwa Waziri aliwakumbusha Wafanyabiashara hao kutumia fursa zilizopo na kuwekeza nyumbani Tanzania, kwa lengo la kuongeza ajira na kuinua uchumi wa nchi.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiongea machache kumkaribisha Mheshimiwa Naibu Waziri Janeth Mbene, kwenye Ofisi za Ubalozi huo zilizopo London. Naibu Waziri Mbene ameondoka usiku wa jumapili tarehe 1 kurejea Tanzania, alikuwa nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi na kutembelea Vituo vya Kibiashara vya Tanzania na Dubai.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Janeth Mbene, akiwa pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Saccoma, Mhe. Waziri alipokutana Viongozi wa Jumuiya hiyo ya Saccoma kuangalia jinsi gani inaweza kushirikiana na Tanzania kuwawezesha Wafanyabiashara wa Tanzania kuleta bidhaa zao nchini Uingereza kama ilivyo kwa Wafanyabiashara wa nchi nyingine za Afrika, ambazo bidhaa zao zimejaa nchini Uingereza tofauti na bidhaa za Tanzania ambazo hazipo. Pichani(kulia) Mheshimiwa Waziri Janeth Mbene, Mama Perez Ochieng (Saccoma - CEO), Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, Mwakilishi wa Saccoma na Dada Magdalena Hall, msaidizi wa Waziri.
 Mheshimiwa Waziri Janeth Mbene(nne kushoto), Naibu Balozi wa Tanzania, Bwana Msafiri Marwa (tano kushoto),wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi, alipokutana nao kwa mazungumzo mafupi kwenye ofisi za Ubalozi, London.

 Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akiwa kwenye Ofisi za Kituo cha Biashara cha Tanzania, London. Pichani kulia ni Bwana Yusuf Kashangwa, Mkurugenzi wa Kituo na Dada Magdalena Hall msaidizi wa Waziri.
 Waziri Janeth Mbene (pili kulia), alipokutana kuzungumza na Wafanyabiashara wa Tanzania waishio nchini Uingereza na baadhi ya Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania. Pichani (kushoto), Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe, Bwana Msafiri Marwa (pili kushoto) na Bwana Khaki, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kitanzania waishio nchini Uingereza.
Naibu Waziri wa Viwanda, Mhe. Janeth Mbene akiongea na Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza Tanzania, alipokutana nao katika Mkutano ambao uliandaliwa na Chama cha Biashara na Wawekezaji wa Afrika kijulikanacho kama Business Council for Africa (BCA). Picha zote na Ally Rashid Dilunga

No comments:

Post a Comment