Wednesday, March 25, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AHUDHULIA KONGAMANO LA KIMATAIFA KUHUSU BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI NCHINI BOTSWANA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa SIR SERETSE KHAMA Nchini Botswana kwa ajili ya kuhudhuria kwenye kongamano la Kimataifa kwa Viongozi wakuu wa Nchi, kuhusu biashara haramu ya wanyamapori Duniani. Kongamano hilo limefanyika leo March 25,2015 kwenye Hoteli ya Mowana iliyopo katika mbuga ya wanyama Kasane Nchini Botswana.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal Mama Zakia Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Afrika ya kusini Mhe. Radhiya Msuya wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa SIR SERETSE KHAMA Nchini Botswana kwa ajili ya kuhudhuria kwenye kongamano la Kimataifa kwa Viongozi wakuu wa Nchi, kuhusu biashara haramu ya wanyamapori Duniani. Kongamano hilo limefanyika leo March 25,2015 kwenye Hoteli ya Mowana iliyopo katika mbuga ya wanyama Kasane Nchini Botswana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal, akimsikiliza Rais wa Botswana Mhe. Seretse Khama alipokua akifungua kongamano la Kimataifa kwa Viongozi wakuu wa Nchi, kuhusu biashara haramu ya wanyamapori Duniani. Kongamano hilo limefanyika leo March 25,2015 kwenye Hoteli ya Mowana iliyopo katika mbuga ya wanyama Kasane Nchini Botswana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal, akiwa na ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano la Kimataifa kwa Viongozi wakuu wa Nchi, kuhusu biashara haramu ya wanyamapori Duniani. Kongamano hilo limefanyika leo March 25,2015 kwenye Hoteli ya Mowana iliyopo katika mbuga ya wanyama Kasane Nchini Botswana. kulia Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal kulia, Rais wa Botswana Mhe. Seretse Khama katikati na Rais wa Gabon Mhe. Ali Bongo Ondimba wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kongamano la Kimataifa kwa Viongozi wakuu wa Nchi, kuhusu biashara haramu ya wanyamapori Duniani. Kongamano hilo limefanyika leo March 25,2015 kwenye Hoteli ya Mowana iliyopo katika mbuga ya wanyama Kasane Nchini Botswana.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano hilo.

Kasane - Botswana
Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi za  Afrika pamoja na wadau wa sekta ya wanyamapori wamekutana nchini Botswana ambapo  wamezungumzia namna ya kukomesha biashara haramu ya  wanyamapori.

Mkutano huo uliofanyika jana (25/3/2015) katika Hoteli ya Mowana iliyoko kwenye Hifadhi maarufu ya wanyamapori ya  Kasane ni matokeo ya mkutano wa London ambako viongozi kutoka nchi mbalimbali walikutana  na kuweka utashi wa kisiasa katika kushugulikia tatizo hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mkutano huo ambapo ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia Tanzania kifedha na teknolojia ili kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori ikiwemo ujangili.

Dkt. Bilal alisema uwindaji haramu ni mtandao mpana unaofanywa kwa siri duniani kote na kusisitiza uhalifu huo unatumia vigezo vya uwezo mdogo wa nchi kifedha na teknolojia duni jambo linalochangia ongezeko la biashara haramu ya wanyamapori.

Makamu wa Rais aliwaambia wajumbe hao kuwa Tanzania inahitaji jumla ya Tshs. Bilioni 20 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbali mbali zenye lengo la kudhibiti biashara haramu ya wanyamapori.

Katika mkutano huo Dkt. Bilal alielezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori ikiwemo  kutunga  sera,kanuni na sheria za kulinda wanyamapori pamoja na kusaini mikataba mbalimbali ya kimataifa yenye lengo la kulinda wanyama hao.

"Kwa Tanzania, Serikali imeimarisha ushirikiano wake na zile nchi ambazo zina mahitaji makubwa ya mazao ya wanyamapori ikiwemo China kwa kusaini makubaliano ya kudhibiti biashara haramu ya wanyamapori," alidokeza Dkt. Bilal.

Aidha, mwezi Novemba 2014, Tanzania iliandaa mkutano wa kanda ya mashariki  ambapo ulipitisha Azimio la Arusha la Utunzaji wa Mazingira na  Udhibiti wa Ujangili. Azimio hilo lilisainiwa na nchi za  Burundi, Kenya, Malawi, Msumbiji, Sudan ya Kusini, Uganda, Zambia na mwenyeji Tanzania.

Kwa upande wa kuzuia ujangili Makamu wa Rais alisema serikali kwa mwaka 2014 imeajiri askari wanyamapori  608 na wale wa kujitolea 300 kusaidia kampeni za kukomesha ujangili na kuongeza kuwa ifikapo Julai mwaka  mwaka huu, serikali itaajiri askari wengine  500 kama moja ya hatua za kupambana na ujangili nchini.

"Katika jitihada hizo hizo, tumekamata makontena ya meno ya tembo ndani na nje ya nchi. Tumefanikiwa pia kuwatia hatiani majangili wengi ambao wanasaidia kutupa habari zinazohitajika kwa ajili ya kupambana na wawindaji haramu; na tumeweza pia kukamata silaha zinazotumika katika uwindaji," alisema Dkt. Bilal.

Baadhi ya viongozi walioshiriki Mkutano wa Kasane ni kutoka  Tanzania, Chad, Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Gabon, Namibia, Vietnam, Zimbabwe na wenyeji Botswana.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Safarini Kasane- Botswana

26/03/2015

No comments:

Post a Comment