Monday, March 9, 2015

KAMATI YA BUNGE HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA (LAAC) YABAINI MAPUNGUFU MAKUBWA UJENZI WA CHUO CHA UALIMU CHA AYALABEE WILAYANI KARATU

Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) Azza Hamad akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Halmashauri ya wilaya ya Karatu.Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Karatu Omar Kwang.
Wajumbe wa kamati hiyo Mh ,Tahuida Nyambo na Yahya Issa wakitizama vitabu ,pembeni kulia ni katibu msaidizi wa kamati hiyo Waziri Kizingiti.
Mjumbe wa kamati ya LAAC,Dastan Mkapa akiwa na Katibu wa kamati hiyo,Dickson Bisire wakifutilia hotuba ya mwenyekiti wa kamati hiyo.
Wajumbe wa kamati ya LAAC,Mh Agustino Masele pamojan na Mh Menrad Kigola wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa wakati wa kika hicho na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Watendaji wa serikali kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha wakifuatilia jambo katika kikao hicho.
Baadhi ya watumishi wa Halamshauri ya wilaya ya Karatu wakiwa katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu,Lazaro Titus akiongozana na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Bunge ya Hesabu za serikali za Mitaa kwenda kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwenyekiti akikagua jengo la Chuo cha Ualimu cha Ayalabee ambacho kinatajwa majengo yake kujengwa chini ya kiwango.
Hili ndio jengo la Chuo cha Ualimu cha Ayalabee kama linavyoonekana sehemu ya Paa lake likiwa tayari limebinyea.
Baadhi ya wananchi walipata fursa ya kutoa madukuduku yao kwa kamati juu ya ujenzi wa Chuo hicho.
Mbunge wa jimbo la Karatu ,Mch Izrael Natse pia akjazia neno katika eneo la Chuo hicho.
Jicho la kamati likaona nyufa za kutosha katika jengo hilo kama anavyoonesha mwenyekiti wa kamati hiyo Azza Hamad.
Maeneo mengine ikabainika kuwa ndiyo yalijengwa siku hiyo wakati kamati inaenda tembelea.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa baahi ya maeneo.
Wajumbe wa kamati wakitizama sehemu ya Paa la jengo hilo.
Kmati ikakagua  Hostel ya wananfunzi ambayo licha ya kukutana na kizuizi cha nyuki bado kamati ilibaini kuwa jengo hilo limejengwa chini ya kiwango pia.
Kamati ikaelekea kukagua majengo mengine ya chuo hicho.
Hali ilikuwa ni ile ile.
Baadae kamati ikafika katika nyumba ya wauguzi na kubaini kuwa licha ya kwamba nyumba hiyo imemalizika bado watumishi wa zahanati hawaishi ndani ya nyumba hiyo na badala yake imetolewa kwa wafanyakazi wa REA,kuweka vifaa vyao .
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Knada ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment