Monday, March 9, 2015

BALOZI WA UINGEREZA NCHI AMTEMBELEA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI OFISINI KWAKE LEO

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akimkaribisha Balozi wa Uingereza nchini Bi Dianna Melrose ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianna Melrose ofisini kwake jijini Dar es Salaam kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo Miundombinu ya Barabara za juu flyovers, madaraja ya chuma mabey bridges na suala zima la kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akisalimiana na Richard Boulter kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimatifa ya Uingereza (Department for International Development) aliyeambatana na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianna Melrose.
Majadiliano yakiendelea kati ya Ujumbe wa Balozi wa Uingereza nchini Bi Dianna Melrose pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli.
Ujumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini, wakwanza kulia ni Balozi wa Uingereza Dianna Melrose, anayefuatia ni Meneja wa Masula ya Biashara na Maendeleo Marie Strain pamoja na Richard Boulter kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimatifa ya Uingereza.Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU)-Wizara ya Ujenzi

No comments:

Post a Comment