Sunday, February 22, 2015

ZIARA YA WAZIRI MKUU YAENDELEA MKOANI IRINGA,PIA AHANI MSIBA WA CHIFU ABDU MKWAWA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Chifu wa Wahehe , Mtwa Adam Mkwakwa wa II wakati alipokwenda nyumbani kwa Chief huyo, Kalenga Iringa Februari 20, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishiriki katika dua mbele ya kaburi la marehemu Chifu Abdu Adam Sapi Mkwawa wakati alipokwenda nyumbani kwa Chifu huyo, Kalenga Iringa kuhani Februari 20, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Chifu wa Wahehe,Mtwa Adam Mkwawa wa II wakati alipokwenda nyumbani kwa Chifu huyo, Kalenga Iringa Februari 20, 2015 kuhani msiba wa baba yake Chifu huyo, Marehemu Chifu Abdu Adam Sapi Mkwawa uliotokea hivi karibuni.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimariji mjane wa Marehemu Chifu Abdu Adam Mkwawa pamoja na watoto wakati alipokwenda kuhani msiba huo nyumbani kwao,Kalenga Iringa Februari 20, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa wilaya ya Kilolo baada ya kusomewa taarifa ya wilaya hiyo Februari 21, 2015. Kushoto ni Mkuu wa koa wa Iringa, Amina Masenza.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakisalimiana na walimu wa sekondari ya Ilula kabla ya kukagua ujenzi wa maabara katika shule hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februri 21, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua moja ya madara ambayo yamegeuzwa kuwa maabara katika Shule ya Sekondari ya Ilula akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 21, 2015. Kitendo hicho hakikumfurahisha na aliagiza kisirudiwe tena sehemu nyingine ngo mapya yajengwe kwa ajili ya maabara.
Mke wa Waziri Mkiuu, Mama Tunu Pinda akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilulawilayani Kilolo ambako Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikagua ujernzi wa maabara na kuhutubia wananchi. Februari 21, 2015.
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua banio katika mradi wa umwagiliaji maji wa kijiji cha Nyanzwawilayani Kilolo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 21, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Meneja Mipango wa Kamouni ya Mawasiliano ya simu ya VIETTEL TANZANIA LIMITED tawi la Iringa, Salvatory Elikidus katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkiuu, Mizengo Pinda katika kijiji Nyanzwa wilayani Kilolo Februari 21, 20154. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Tawi la Iringa, Tran Nhat Duy na wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Fedha, Vo Ngoc Thang.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na watoto baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyanzwa wilayani Kilolo akiw akatika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 21, 2015.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akizungumza na Mwenmyekiti Msataa wa Umoja wa Wazazi Tanzania, Abdallah Issa katika kijiji cha Nyanzwa, Kilolo baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhutubia mkutano wa hadahara katika jijiji hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februar21, 2015. (Picha nas Ofiosi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment