Tuesday, February 3, 2015

MBUNGE MGIMWA ACHANGIA VICOBA TANANGOZI ,ASEMA NDOTO YAKE KUWA NA BENKI YA WANANCHI WA JIMBO LA KALENGA

Wanachama  wa  kikundo cha  VICOBA cha  Lukindo woman Group wakimvisha  mavazi ya uchif mbunge wa  jimbo la kalenga Bw Godfrey Mgimwa baada ya  kufurahishwa na jitihada zake  jimboni  humo
Wanachama  wa  VICOBA  Tanangozi  Kalenga  wakimshangilia mbunge  wa  jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa
Mbunge wa   jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa katikati akipokelewa kijiji cha Tanangozi wakati  wa harambee ya  kuchangia VICOBA
Mbunge  Mgimwa  akivishwa  vazi la  kichifu

Mbunge wa  Jimbo la kalenga  Godfrey Mgimwa akiwashukuru  wananchi wa Kalenga kwa  kuendelea  kumuunga mkono katika utendaji wake
Mbunge wa  jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa akizungumza  jambo na mmoja kati ya  watoto  wa wanachama wa kikundi cha VICOBA cha Lukindo Tanangozi
Mbunge  Mgimwa akiondoka  kijiji  cha Tanangozi baada ya  kumaliza shughuli ya  harambee  kijijini hapo
Mbunge  wa jimbo la kalenga  Godfrey Mgimwa akiwa katika  picha ya pamoja na  wanachama wa VICOBA  wa kikundi cha Lukindo
 Na matukiodaimablog

 MBUNGE wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godrey Mgimwa achangia zaidi ya Tsh milioni 1.7 vikundi vya VICOBA kijiji cha Tanangozi huku akidai kuwa uwezekano wa kuanzishwa kwa benki ya wananchi wa jimbo la kalenga upo iwapo mwamko wa wananchi kujiunga katika vikundi vya VICOBA utaendelea kwa kasi kama ilivyo sasa . 

Akizungumza na wanachama wa vikundi hivyo vya Slic na Lukundo woman Group mbunge Mgimwa alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuona jimbo hilo la Kalenga linaendelea kuwa na vikundi vingi zaidi vya VICOBA kama safari ya kuelekea kuwa na Benki ya wananchi wa jimbo la Kalenga ambayo itawawezesha wananchi hao kujikwamua kiuchumi. 

Alisema kuwa jimbo la kalenga ni moja kati ya majimbo ambayo ardhi yenye rutuba na kikwazo kikubwa za wananchi kunufaika na ardhi hiyo ni pamoja na kukosekana kwa taasisi ya kifedha ambayo itasaidia kuwakopesha wakulima fedha za pembejeo na kuwa ndoto yake ni kuona jimbo hilo linakuwa na benki itakayowaunganisha wananchi hao .

 "Moja kati ya ndoto yangu ni kuona jimbo letu la Kalenga linafanikiwa kuwa na benki ya wananchi wa Kalenga ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kusukuma mbele maendeleo ya jimbo hilo kwa kutoa mikopo zaidi kwa wananchi na safari ya kufanikisha kuwa benki hiyo imeanza na iwapo mtanichagua mwaka huu katika uchaguzi mkuu nawahakikishieni kufanya mambo makubwa zaidi ya haya ambayo nimefayanya kwa muda wa mwaka huu moja mlionichangua"alisema Mbunge Mgimwa 

Kuwa wananchi wa jimbo la Kalenga hawana sababu ya kuendelea kuhangaika na wale wanaojipitisha kwa kutaka ubunge kwani kwa upande wake bado ana ndoto ya kutumia uwezo wake wote kuona Kalenga inabadilika kimaedeleo kama ambavyo mbunge aliyepita marehemu Dr Wiliam Mgimwa alivyoanza kwa kasi kusogeza maendeleo kwa wananchi wake. 

 " Ndugu zangu hadi sasa bado mwaka mmoja wa ubunge wangu sijamaliza hadi April mwaka huu ndio nitakuwa nimefunga mwaka mmoja toka nilipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mdogo ila pamoja na muda mfupi ambao nimekuwepo madarakani nina mengi nimefanya ambayo najivunia na kila mwana kalenga amekuwa shahidi katika maendeleo ambayo nimeyaleta " 

Kazi ambazo nimezifanya ni nyigi zaidi mfano suala la umeme katika kata mbali mbali za jimbo hilo ,huduma ya maji safi kuchangia uanzishwaji wa ViBOBA ,Mabati ,Saruji katika miradi ya kimaendeleo inayoanzishwa na wananchi pamoja na miradi mingine mingi ambayo kila mmoja wetu amekuwa akishuhudia haya.

No comments:

Post a Comment