Tuesday, January 27, 2015

UJUMBE KUTOKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI (NDC) WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto) akisalimiana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 27, 2015(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto) akisaini katika kitabu cha wageni mapema leo alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza kwenye ziara ya mafunzo kuhusu uendeshaji wa Jeshi la Magereza(kulia) ni Kamishna wa Magereza, Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwasilisha mada yake ya uchokozi kuhusu Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele ya Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(hawapo pichani).
Wakufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
 
Kamishna wa Magereza, Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania walipofanya ziara ya mafunzO(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Bregedia Jenerali Sylivester Minja.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment