Friday, January 9, 2015

UGENI WA MTEMVU KUTOKA MAREKANI WAFANYA ZIARA YA KIHISTORIA YA MAFUNZO KATIKA MAENEO MBALIMBALI JIMBO LA TEMEKE

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu na mkewe Mariam Mtemvu na Binti yao Sitti Mtevu -kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na wagteni wao kutoka vyuo vikuu viwili vya Marekiani vya State University of New York na University  of Buffalo, baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, leo kuanza ziara yao ya siku mbili katika jimbo hilo, kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya kijamii na maendeleo. Kulia ni Mkuu wa Msafara huo Mtanzania, Profesa Dan Nyaronga wa Chuo Kikuu cha Buffalo nchini Marekani.
 Mtemvu akiwa na mdau wa maendeleo katika jimbo loa Temeke, Fiona Barretto wakati wa mapokezi ya ugeni huo kwenda wa mkuu wa wilaya ya Temeke
  Profesa Dan akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Temeke, baada ya ujumbe huo kukutana na mkuu huyo wa wilaya,  Sophia Mjema, wa pili kushoto,
 Mkuu huyo wa wilaya akizungumza
 Ugeni huo kutoka Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Temeke leo
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo akisalimiana na Binti wa Mtemvu, Siti Mtemvu wakati msafara ulipoingia ofisini kwa mkurugenzi huyo leo
 Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja ana viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
 Wanahisa wa Mfuko wa wa Kupambana na Umasikini Temeke -TFP,  wakiulaki ugeni wa Mtemvu na Wamarekani hao ulipowasili kwenye Ofisi za TFP leo
Mtemvu akizungumza na wadau wa PFT
 Profesa Dan Nyaronga akizungumza na wadau wa mfuko huo  wa PFT
 Binti wa Mtemvu Sitti akisalimia wanachama wa mfuko huo
 Mtemvu na ugeni wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Mfuko wa PFT baada ya mazungumzo ya kubadilishana uzoefu wa anamna ya kuondoa aumasikini katika jamii
 Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, akiwa na baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vikuu hivyo ya Marekani ambao ni miongozi mwa waliokuwa katika ugeni huo wa Mtemvu, hapa ilikuwa kwenye ofisi za PFT.
 Mbunge wa Temeke, Mtemvu akipata chakula cha mchana na ugeni wake katika hoteli ndani ya jengo la Quality Centre
 Maofisa katika Ofisi ya Mbunge wa Temeke, wakaiwa kwenye hoteli wakati wa chakula hicho cha mchana.
 Polisi wa usalama barabarani akiongoza msafara wa ugeni huo kutoka Quality Plaza kwenda Hispitali ya Rufani ya mkoa wa Temeke kuendelea na ziara
 Ugeni ukipata maelezo mbalimbali katika ukumbi wa hospitali hiyo
 Msafara ukitoka ukimbini baada ya mazungumzo hao. Kulia ni Mgaga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Temeke, Dk. Amaani Malima
 Dk. Malima akitoa maelezo kwa wageni hao katika chumba cha kujifungulia kwa upasuaji
 Dk. Malima akiendelea kutoa maelezo kwa ugeni huo
 Binti wa Mtemvu Sitti Mtemvu akigawa chandarua kwa Devota Boniface,  mama mzazi aliyejifungua katika hospitali hiyo ya Temeke.,

 Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa hospitali hiyo ya Temeke. Kulia ni Mgaganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk. Sylvia Mamkwe.
Watoto katika kituo cha watoto yatima cha Makao, Kurasini,Temeke Dar es Salaam, wakisubiri ugeni huo wa wamarekani, ulipowaili kwenye kituo hicho.
 Mmoja wa wageni kutoka Marekani Leanne Thomas wa State University of Buffalo, akifurahia kuchezea nyoka wakati kikundi cha ngoma cha Sanaa cha Hisiaa Theatre Group kwenye kituo hicho cha yatima, Kurasini
 Mtemvu akijitwisha nyoka kujaribu kama walivyokuwa wakifanya wasanii wa kikundi hicho cha sanaa
 Profesa Dan Nyaronga naye akijitwisha nyoka
 Mmmoja wa wageni hao kutoka Marekani akishangilia baada ya kubebeshwa nyoka na wasanii wa kikundi hicho cha ngoma
 Mmoja wa wanafunzi akibeba nyoka ya wasanii hao
 Mtemvu, mkewe na mtoto wao Sitti wakifurahia kubeba nyoka wa kikundi hicho cha sanaa
 Mtemvu na msafara wake wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kikundi hicho cha sanaa
 Mama mlenzi wa kituo cha Makao ya watoto wenye shida cha Kurasini, Betrice Mgumiro akizungumza wakati Mtemvu na ugeni wake walipitembelea kituo hicho
 Sitti Mtemvu akimkabidhi chandarua mtoto kwenye kituo hicho cha Makao cha watoto wenye shida
 Profesa Dan akikabidhi chandarua kwa watoto wa kituo hicho
 Laurien Martinek wa Marekani ambaye yupo katika msafara huo wakigawa chandarua kwa Fatuma  Jabiri wa kikundi hicho cha sanaa
 Mdau wa maendeleo jimbo la Temeke, Fion Barretto akigawa chandarua kwa msanii huyo
 Sitti akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliogawiwa chandarua
 Mtoto Baraka Rashid, kutoka kituo cha watoto wenye shida cha Kurasini akitoa shukrani baada ya ugeni kugawa vyandarua kwa watoto kadhaa
 Ugeni ukionyeshwa mifungo kwenye kituo cha watoto yatima kwa ajili ya kitoweo
 Mmoja wa wageni hao akichukulia ndani ya jengo ambalo limebaki gofu kutokana na kutokuwa na vifaa mbalimbali vya kujifundishia ufundi ikiwemo vyerehani. Picha zote na Khamisi Mussa

No comments:

Post a Comment