Saturday, January 24, 2015

RAIS WA TFF JAMAL EMIL MALINZI ATEMBELEA UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA LEO

Na Faustine Ruta, Bukoba
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Emil Malinzi wa pili kutoka (kushoto) akiongozana na Baadhi ya Viongozi wa Mpira hapa Nchini leo hii Mchana alipowasili katika Uwanja wa Kaitaba unaokarabatiwa kuwekwa Nyasi za Bandia. Bw. Jamal Emil Malinzi pia ndie Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) alipowasili hapa Bukoba amezungumza na Viongozi wa Soka Mkoani hapa Kagera na baadae.
Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi pia aliambatana na Viongozi mbalimbali hapo Uwanjani akiwemo Bw. Pelegrinius A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF makao makuu, Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama ambaye pia ni Kiongozi kamati ya Waamuzi Nchini.
Doron Mommsen(kushoto) akiongea na Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi(kulia) leo wakati Rais huyo alipotembelea kujionea Ukarabati huo wa Uwanja wa Kaitaba ambao Utachukua Muda wa Miezi Mitatu. Meneja wa Mradi Bw. Doron Mommsen amemweleza Ndugu Jamal Malinzi kwamba Ukarabati unaendelea Vizuri na kinachoendelea kwa sasa ni kusawazisha Udongo katika Uwanja huo.
Meneja wa Mradi Bw. Doron Mommsen akionesha kile kinachoendelea atika Uwanja huo wa Kaitaba.
Meneja wa Mradi Bw. Doron Mommsen akishukuriwa na Rais Jamal Malinzi Uwanjani hapo Kaitaba baada ya kumwelezea kwa kirefu katika Ujenzi huo wa Uwanja.
Dreva akiendelea na kazi yake Katika Uwanja akishindilia Udongo ili waweze kupata Usawa.
Picha ya Pamoja Meneja wa Mradi Bwana Doron Mommsen (katikati) Rais wa TFF Bwana Jamal Malinzi, Viongozi na Wafanyakazi
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Emil Malinzi.

No comments:

Post a Comment