Friday, January 30, 2015

MKURUGENZI MKUU WA NHC AENDELEA NA ZIARA YAKE MIKOANI

Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana cha Mshikamano Wilayani Muleba alipokitembelea kuona namna kinavtumia mashine zilizotolewa na NHC ili kuongeza ajira kwa vijana. Bw. Mchechu amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuunga mkono juhudi za NHC kwa kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia kazi zao.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Mtukula linapojengwa jingo la kisasa la biashara na NHC ili kuvutia na kuchochea ukuaji wa biashara katika eneo hilo la mpaka wa Tanzania na Uganda. Eneo hili ndipo zilipokuwa nyumba ndogondogo zilizojengwa na NHC na baadaye kuharibiwa na mabomu ya Nduli Iddi Amin alipovamia nchi yetu mwaka 1978. NHC iliiomba  Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kulirejeshea eneo hilo ili kujenga jengo hilo la kibiashara
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua viwanja vya NHC Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu ikiwa ni program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za makazi za NHC Wilayani Chato alipotembelea Wilaya hiyo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akimpa maelezo Mjumbe wa Bodi ya NHC Bi Subira Mchumo ya juhudi  zinazofanywa na NHC katika Halmashauri mbalimbali za Wilaya nchini za kuwapatia wananchi makazi bora. Ujumbe huo ulitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba na kusisitiza matumizi ya malighafi zinazopatikana katika maeneo husika ili kupunguza gharama za nyumba hizo.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika Wilaya ya Muleba kwa ajili ya kuuzia wananchi. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho ya ukamilishaji.
 Msanifu wa Majengo wa NHC Bw. Kintu akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ya jengo linalojengwa na NHC eneo la Mtukula ili kukuza biashara upande wa Tanzania.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ulipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kujionea juhudi zinazofanywa na mwekezaji wa kiwanda hicho katika kutoa ajira kwa watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Kiongozi wa kikundi cha vijana kilichoko Wilaya ya Bukoba Mjini waliyofadhiliwa na NHC mashine za kutengezea matofali  ili kujipatia ajira

No comments:

Post a Comment