Sunday, January 11, 2015

Mh. Makalla akagua miundombinu ya maji jijini Mbeya

Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi jijini Mbeya na kufanikiwa kutembelea vyanzo mvali mbali vya maji vilivyo chini ya Mamlaka ya Maji Safi jijini humo.

Mh. Makalla amevutiwa sana na utendaji kazi wa Mamlaka hiyo na kuupongeza kwa kuongeza idadi kuwa wateja wa maji kutoka 9000 mwaka 2002 na kufikia 40,000 hivi sasa na pia kuwa mamlaka ya tatu kitaifa kuwa na miundombinu ya majitaka.

Mh. Makalla ameiagiza Mamlaka hiyo kuhakikisha inadhibiti upotevu wa maji kutoka asilimia 34 ya sasa na wafikie kiwango cha kimataifa asilimia 20.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla  (katikati) akimsikiliza Ing. Martin Kimambo wakati akimwonyesha na kumpa maelezo kuhusu miundombinu ya maji taka eneo la Kalobe.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akiangalia chujio la maji eneo la Swaya.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla  akishuka kwenda kukagua tanki la maji la kadege,jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akishuka kukagua mitambo eneo la Kadege.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akielekeza jambo wakati akikagua chanzo cha chemchem Nzovwe.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akimsiliza mwenyekiti wa bodi ya maji jijini Mbeya,Jaji Atuganile Ngwale.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akiongea na bodi na Menejimenti ya Mamlaka Maji jiji la Mbeya.

No comments:

Post a Comment